Mshambuliaji wa Argentina na nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Lionel Messi ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa.
Maamuzi hayo magumu kwa Messi yamekuja ikiwa ni muda mchache baada ya timu yake kushindwa kutwaa kombe la Copa America mbele ya Chile ambapo wamekubali kufungwa kwa mikwaju ya penati ya 4-2.
Akizungumza baada ya fainali hiyo Mesi amesema “Haimaanishi kwangu. Mimi na timu ya taifa nimemaliza”
“Nilikuwa na fainali nne, nilijaribu , lilikuwa ni jambo ambalo nilikuwa nikilihitaji sana lakini sikupata, kwahiyo nadhani nimemaliza”
Baada ya kutangaza, Messi amestaafu kwa kaucha rekodi katika timu ya taifa ya Argentina kwa kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi 55, rekodi ambayo bado haijafikiwa na mchezaji mwingine wa timu ya taifa ya Argentina.