Jumamosi, 25 Juni 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AFUTURISHA MAKUNDI MBALIMBALI YA VIONGOZI, WALEMAVU WA NGOZI, WASIOJIWEZA PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

 Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli amefuturisha makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu wa ngozi Albino, Wavuvi wa ferry, walemavu vya viungo pamoja na wafanyakazi wa Ikulu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir wakati wakielekea kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir mara baada ya kufuturu na makundi ya watu mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na makundi mbalimbali (hawapo pichani)ikiwemo viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu wa ngozi (Albino),walemavu wa viungo pamoja na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir  , Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum pamoja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakiwa wamesimama wakati wa dua mara baada ya kufuturu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye foleni ya kupata futari pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Ikulu jijini Dar es Salaam.
Continue reading →

0 maoni:

Chapisha Maoni