Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki akatika Mkutano wa Viongozi Wakuu
wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika ( SADC) uliofanyika kwenye hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone
Botswana Juni 28. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli
kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU wa Lesotho, Dk.
Pakalitha Mosisili amekubali kutekeleza masharti yaliyowekwa na Wakuu wa
Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya
Uchumi na Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), na kuridhia timu ya uchunguzi kwenda nchini humo kufanya uchunguzi wa hali ya kiusalama na kisiasa.
Dk. Mosisili ametoa uamuzi huo
leo (Jumanne, 28 Juni, 2016) wakati wa kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na
Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa,
Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security
Cooperation) kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
(GICC), jijini Gaborone, Botswana.
Pia amekubali viongozi waupinzani
na baadhi ya maofisa wa kijeshi wanaoishi uhamishoni ambao walikimbia
machafuko yaliyotokea nchini humo warejee nchini mwao na kuahidi kwamba
atahakikisha wanapatiwa ulinziwa kutosha.
Januari mwaka huu, mkutano wa
SADC Double Troika uliagizakwambaifikapo Februari Mosi, mwaka
huuSerikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa
kuchunguza matatizo ya kisiasa na kiusalama nchini humo hususan
mazingira yaliyopelekea kifo cha marehemu Luteni Jenerali Maaparankoe
Mahao ambaye alikuwa Mkuuwa Majeshi.
Kwaupande wake, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe
Magufuli katika kikao hicho amesema wamepitia ripoti iliyoundwa na timu
ya SADC iliyochunguza kuhusu matatizo ya Lethoto ambayo iliwahoji
Viongozi wa Serikali, Jeshi, Bunge na familia ya marehemu Luteni
Jenerali Mahao.
“Lengo la hatuahiiza SADC ni
kuhakikisha inarejesha hali ya amani na utulivu kwenye maeneo ya siasa,
ulinzi na usalama katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili wananchi
wake waweze kuishi vizuri,” amesema
Pia Waziri Mkuu amesema Tanzania
inatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Wakuu wa Nchina Serikali na Kamati
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), Agosti mwaka huu ambapo kitafanyika kikao kingine nchini Tanzania.
Mkutano huo wa ulifunguliwa na
Rais wa Botswana, Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama na ulihudhuriwa
na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk.
John Pombe Magufuli; Rais wa Afrika Kusini, Bw. Jacob Zuma; Rais wa
Msumbiji, Bw. Filipe Jacinto Nyusi; Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe,
Mfalme Muswati wa III wa Swazland.
SADC Double Troika ni
kikao maalum kinachojumuisha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na
wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ
on Politics, Defense and Security Cooperation).
SADC Double Troika ni
mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha
ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye
Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha
mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na
mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.
Chini ya muundo wa SADC, kuna
mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao
unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la
siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC
Organ).
Wajumbe wa mkutano wa SADC Organ
ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda
wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo
Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaunda SADC Summit.
0 maoni:
Chapisha Maoni