Jumatatu, 27 Juni 2016

SERENGETI BOYS YAONGOZA GOLI 3-0 DHIDI YA SECHELLES UWANJA WA TAIFA,MPIRA UNAENDELEA.


b Mpira umeanza kwa kasi na katika dakika 10 za mwanzo Serengeti Boys wanaonekana kutawala mpira na katika dakika ya 15 Nickson Kibabage anaiandikia Serengeti goli la kwanza akitumia maridadi mguu wake kushoto na kutinga nyavuni.
Dakika ya 22, Ibrahim Ally anaiandikia Stars goli la pili ikiwa ni shambulizi lililoanzia katikati ya uwanja.Mpira  umeonekana kuchezwa upande mmoja na Serengeti kukosa nafasi nyingi za  wazi.Mpira ni mapumziko na Serengeti wanatoka wakiwa mbele kwa goli 2.
Kipindi cha pil kimeanza na timu zote kuwa makini ambapo dakika ya 60, Ally Msengi anaiandikia Serengeti goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Shelisheli kuushika ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru penati.
Mchezo kati ya Serengeti Boys na Sechelles unaopigwa hivi sasa uwanja wa  Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza kwa bao 3-0. 
hhWachezaji wa timu ya Serengeti Boys wakishangilia mara baada ya kupata goli. 
rrMchezaji wa timu ya Serengeti Boys Rashid Mohamed Chambo akimchomoka  mchezaji wa timu ya Sechelles,katika mchezo wao unaopigwa hivi sasa  uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza  bao 3-0.
tWachezaaji wa timu ya Serengeti Boys wakionesha umahiri wao dhidi ya timu ya Sechelles.
wsMchezaji wa timu ya  Sechelles akiwa amelelala chini katika nginja ngija ya kusaka magoli dhidi ya timu ya Serengeti Boys ,katika mchezo wao unaofanyika hivi sasa uwanja wa  Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza bao 3-0.
Picha kwa hisani ya Michuzi Blog

0 maoni:

Chapisha Maoni