Baadhi
ya vijana wanaounda kundi la Mkubwa na Wanawe Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Temeke wakati wa tukio hilo lililofanyika leo Juni 26.2016
Kiongoni
wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, akielezea namna vijana wake
walivyoguswa na kuamua kujitolea kwa ajili ya watu wenye kuhitaji
wakiwemo wa Hospitali hiyo ya Temeke.
Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, akimkabidhi baadhi ya vifaa Daktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage
Baadhi ya wasanii wa kundi la Yamoto Band ambao pia wanatoka Mkubwa na Wanawe wakitoa vionjo kadhaa wakati wa tukio hilo.
Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella akishukuru kwa hatua hiyo ya kurudisha fedhila kwa Jamii
Msanii
Kiongozi wa Kundi la Yamoto Band,"Aslay Isihaka"-Dogo Aslay akizungumza
kwa niaba ya wasanii wenzake wa Yamoto pamoja na kundi hilo la Mkubwa
na Wanawe
Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella akionyesha moja ya vifaa hivyo vya tiba
Daktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage akionyesha moja ya kifaa huku akielezea namna kinavyofanya kazi
Makabidhiano yakiendelea..
Vijana na Mabalozi wa kundi la Mkubwa na Wanawe wakibeba baadhi ya vifaa walivyotoa msaada hospitalini hapo.
Wakielekea wodini...
Amani James a.k.a Chiba wa kundi la Yamoto Band akitoa msaada katika tukio hilo
Msanii
Kiongozi wa Kundi la Yamoto Band,"Aslay Isihaka"-Dogo Aslay akimfariji
mmoja wa Watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Temeke
Said Fella (kulia) na Mh. Temba (kushoto) wakielezea jambo wakati wa tukio hilo leo Juni 26
Enock Deogratius 'Enock Bella' akimfariji mtoto
Amani
James a.k.a Chiba wa kundi la Yamoto Band aliweza kuwafariji watoto na
ndugu wanaouguza watoto wao pale walipomuomba awachezee kidogo kwani
imekuwa faraja kwa kumuona kwa mara ya kwanza
Mkubwa na Wanawe..
Mkubwa na Wanawe
Baadhi
ya vijana wanaounda kundi hilo la Mkubwa na Wanawe wakiwa katika picha
ya pamoja wakati wa tukio hilo la kutoa msaada hospitali ya Temeke. leo
Juni 26.2016. (Picha zote na Andrew Chale
Kituo
cha kuvumbua na kuendeleza vipaji vya muziki cha Mkubwa na Wanawe,
kimetoa msaada ya vifaa vya tiba na vifaa mbalimbali vikiwe vile vya
usafi, dawa za meno, sabuni, maji na juisi kwa wodi ya Watoto waliolazwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Jijini Dar es Salaam.
Awali
akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, kiongoni wa kituo hicho,
Said Fella, amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na
changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ya Temeke ambayo pia ni majirani
zao ambapo pia amebainisha kuwa kundi hilo limekuwa likifika
Hospitalini hapo kuchangia misaada mbalimbali.
Said
Fella ameongeza kuwa, alishauriwa na vijana wake waliopo katika kituo
chake kuona ni vipi wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kijamii
kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na wote kwa
pamoja kukubaliana kutoa msaada huo.
“Nasi
pia ni kama wagonjwa watarajiwa, hivyo tumeona ni vema kuja kutoa
msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kama tulivyoshauriwa na wenyeji
wetu, tukiwa pamoja na mabalozi wetu. Msaada tuliotoa una thamani ya Sh
milioni tatu,” alisema Fella.
Akipokea
msaada huo, mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage,
alikishukuru kituo hicho kwa kuwakumbuka akiwataka wasanii na viongozi
wake pamoja na wengineo wenye nafasi kuendelea kuwakumbuka.
“Vifaa
tulivyoletewa ni Paso-Oximeter cha kupimia kiwango cha oksijeni
mwilini, HB Culvate cha kupima kiwango cha damu, mashine ya BP ambayo
kazi yake ni kufahamu kama presha ya damu (BP) imeshuka au la na Mashine
ya Nebulizer yenye kazi ya kuwapimia dawa wagonjwa wa pumu,” alisema
Nyumbiage.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake takribani 50 alioambatana nao hospitalini hapo,
msanii anayeunda kundi la Yamoto, Dog Aslay, alisema kuwa wamefarijika
kuwasaidia wagonjwa akiahidi kufanya hivyo wakati mwingine watakapopata
nafasi.
Tukio
hilo la aina yake kwa kundi hilo ambalo ufanya mara kwa mara katika
kutembelea jamii na kusaidia misaada, limeweza kupongezwa na baadhi ya
ndugu wa wagonjwa na wagonjwa wenyewe kwa kueleza kuwa ni tendo la
kuigwa na kila mmoja wetu hasa wasanii ambao ni kioo cha jamii.
0 maoni:
Chapisha Maoni