Wanajeshi
wa Sudan Kusini waliokuwa wenye njaa wameiba chakula kutoka kwa
mfanyibaishara mmoja katika moja ya masoko makuu kwenye mji mkuu wa nchi
hiyo Juba.
Wakati
mfanyibiashara huyo katika soko la Konyo Konyo aliwataka wanajeshi hao
walipie chakula hicho, walimjibu na kumuambia aende kwa Rais Salva Kiir
kudai pesa zake kwa sababu hawajalipwa mishara kwa miezi kadha.
Wafanyibiashara wengine walifunga maduka yao ili wanajeshi hao wasije nao wakawaibie.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni