Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu katika tukio la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa
habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri
Jijini Dodoma. Katika tukio hilo Dk. Tulia Ackson alichangia kiasi cha
shilingi milioni moja.
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto), Msanii wa
Bongo Movie, Aunt Ezekiel (kulia) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian
Kamazima (katikati) wakiosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa
habari nchini. |
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia)
akiosha gari na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kushoto)
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa
habari nchini. Katika tukio hilo Dk. Hamisi Kigwangalla alichangia
shilingi milioni moja. |
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiosha gari
katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya
waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa
Jamhuri Jijini Dodoma. |
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kulia) akiosha moja
ya magari ya wabunge kuwaunga mkono waandishi wa habari katika tukio la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa
habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri
Jijini Dodoma. |
|
Mwenyekiti wa Bunge Sports,
William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza
waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car
Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia ni Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson
Mwansasu na Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari
‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson (katikati). Katika zoezi
hilo Ngeleja alichangia shilingi laki moja huku timu ya bunge ikichangia
shs milioni moja. |
|
Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa
Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin
Thompson (katikati) akizungumza katika zoezi la kuosha magari kwenye
kampeni maalumu ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash
For Health’ ikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia
bima ya afya waandishi wa habari nchini. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson na Mwenyekiti wa
Bunge Sports, William Ngeleja (kushoto). |
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kulia)
akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi
wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri
Dodoma. Dk. Tulia alichangia shs milioni tano. |
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto) akiosha
moja ya magari ya wabunge kuwaunga mkono waandishi wa habari katika
tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi
wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri
Jijini Dodoma. |
|
Mmoja wa wasanii wa muziki
akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha
fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. |
|
Mmoja wa wasanii wa muziki
akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha
fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. |
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati)
akimkabidhi hudi ya shs milioni moja Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa
Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin
Thompson (kushoto) kwa ajili ya kuchangia fedha kuwakatia bima ya afya
waandishi wa habari nchini. Kulia ni Mratibu wa zoezi hilo. |
|
Miss Tanzania 2014/15, Lilian
Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kushoto) wakijitolea kuosha magari
kwenye kampeni hizo. NHIF waliosha gari lao kwa shs 100,000/-.
…………………………………………………………………………….
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki harambee ya
kuchangia waandishi wa habari kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya “Media
Car Wash For Health” iliyofanyika leo katika viwanja vya Jamhuri Mjini
Dodoma ambapo amechangia jumla ya shilingi milioni 5 ili kuokoa maisha
ya waandishi wa habari.
“Kuna umuhimu mkubwa wa kuwachangia waandishi wa habari kwani
wamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya nchi na
kuhamasisha amani ya nchi, kwa kutambua umuhimu wao nitachangia shilingi
5,000,000 ili iweze kuwakatia Bima ya Afya,” alisema Mhe.Dkt. Tulia.
Licha ya kuchangia fedha hizo Mhe. Tulia aliosha baadhi ya
magari ya waheshimiwa wabunge kwa ajili ya kuchangia harambee hiyo
ambapo kila mbunge aliyeoshewa gari yake alichangia shilingi 100,000
ambazo moja kwa moja ziliingia katika mfuko wa kuokoa maisha ya
waandishi wa habari kwa kuwakatia Bima ya Afya.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendelea ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla amechangia shilingi
1,000,000/= ambayo nayo inaenda kusaidia waandishi wa habari ili waweze
kukatiwa Bima ya Afya.
Lengo la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni
200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya afya zaidi ya waandishi wa
habari 1000 hapa nchini. Aidha harambee hii ni ya pili, harambee
nyingine kama hii ilifanyika mwaka 2015, viwanja vya Leaders jijini Dar
es Salaam na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidia
kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa wanaugua kwa kipindi
kirefu. |
0 maoni:
Chapisha Maoni