Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki akiongea na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao
(eGA) (hawapo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye
ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms
mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari
akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki ili aweze kuzindua Baraza la
Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la
Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah
KairukiMwenyekiti
wa TUGHE tawi la Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Long’ida Oltetiai
akitoa taarifa ya tawi hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati
wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo
Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Angellah Kairuki.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA)
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la
Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la
Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa
Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya
uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
——————————————————-
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Watumishi
wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wameaswa kuweka vipaumbele na
mikakati ya kusimamia mifumo ya TEHAMA inayoboresha utendaji kazi na
kutoa huduma ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ndani ya
Serikali.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua
baraza la wafanyakazi la Wakala hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es
salaam.
“Nataka
mbuni na kutengeneza mifumo tumizi mipya pamoja na kuiboresha mifumo
tumizi iliyopo ili kuongeza tija kwenye sekta za kimkakati hususan sekta
za afya, kilimo, utalii, elimu, viwanda na biashara” alisema Kairuki.
Waziri
Kairuki aliyataja maeneo mengine ambayo yanapaswa kuboreshwa katika
ukusanyaji na kutiliwa mkazo katika ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja
na sekta za fedha, rasilimaliwatu, ardhi na utambulisho wa taifa.
Hatua
hiyo ya eGA ya kuboresha mifumo ya TEHAMA itasaidia Serikali kuimarisha
uwezo wake wa kuwa na taarifa juu ya mifumo yake na kukidhi mapato yake
na amewataka watumishi hao wazidishe kasi ya utendaji kazi ili kuendana
na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”.
Aidha,
watumishi hao wamesisitizwa kuwa kuundwa kwa baraza hilo la wafanyakazi
ni moja ya nyenzo ya kuishauri Serikali katika ngazi ya taasisi katika
usimamizi wa kazi na rasilimali, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki
na wajibu waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora
za kazi na maslahi na kusimamia haki na usatawi katika sehemu za kazi.
Akizungumzia
utendaji kazi wa Wakala hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa hatakubali
kuona Wakala hiyo kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye utendaji kazi wa kila
siku bali watumishi wafanye kazi kwa weledi na kuwa na mchango katika
kuzipatia suluhisho changamoto zinazoikabili Serikali kwa sasa.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt.
Jabiri Bakari alipokuwa akimkaribisha Waziri mwenye dhamana ya Utumishi
wa Umma alisema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi ambapo hadi sasa wanatumia gharama kubwa
katika kukodisha jengo ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Dkt
Bakari alitaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la tishio la usalama
mtandaoni kutokana na ukweli kuwa kadiri Serikali inavyozidi kuhamia
mtandaoni, hali ya uhalifu nayo inahamia mtandaoni.
Katika
kutimiza majukumu yake, hadi sasa Wakala ya Serkali Mtandao ina
wafanyakazi wapatao 94 ambapo inatarajiwa kuwa jumla ya watumishi 126
mara Serikali itakapotoa kibali cha kuajiri watumishi wapya.
Wakala
hiyo imejenga historia mpya ya kuwa na viongozi wa kwanza wa baraza
hilo ambapo Donald Samwel amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kwa kura 29
zilizopigwa za wajumbe wakati Dianah Mlokozi naye ameingia kwenye
historia hiyo kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
Baraza
la wafanyakazi la eGA limezinduliwa kwa mujibu wa kutekeleza Sera ya
kuwakilisha wafanyakazi mahala pa kazi kkama ilivyoelekezwa kwenye
sheria ya majadiliano katika utumishi wa Umma na sheria ya ajira na
mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004.
0 maoni:
Chapisha Maoni