Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitazama madawati yaliyokamilika kulia ni afisa habari wa Manispaa ya Iringa Sima Bingileki |
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo kulia akipokea madawati kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Iringa |
Mwakilishi wa mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi Hawa akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Masenza mara baada ya kukabidhiwa madawati |
Na Esta Malibiche.blogspot.com |
Serikali mkoani Iringa imetekeleza
agizo la Mh.Rais Dr.John Magufuli aliyowaagiza wakuu wa mkoa nchini,kuhakikisha
ifikapo tarehe 30/6/2016 wawe wamekamilisha mawadati katika shule zenye uhaba.
Akikabidhi madawati kwa wakurugenzi wa wilaya mkoani hapa, Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema serikali
yake imetengeneza madawati 21 ,304 kwa ajili ya shule za Msingi na
madawati 3,665 kwa ajili ya Shule za Sekondari.
Masenza aliongeza kuwa madawati 8,163
kwa ajili ya Shule za Masingi na mengine 1,264 kwa ajili ya Shule za Seondari
bado yanatengenezwa katika karakana mbalimbali na kweamba pindi
yatakapokamilika yatafanya mkoa huokuwa na ziadi ya madawati badala ya
upungufu.
Alisema kuchelewa kukamilika
kwawakati kwa kazi ya kutengenezamadawati katika katika Halmashauri mbalimbali
mkoani hapa kulitokana na wakandarasi wanaotengenezaa madawati kuwa na
kazinyingi.
Hata hivyo alifafanua kuwa Madawati
yaliyobaki kwa Halmashauri za Manispaa ya Iringa,Kilolo,Mufindi,Wilaya ya
Iringa yanatarajia kukamilika kati ya Julia 3 na 15 huku Halmashauri ya Mji wa
Mafinga ikitarajia kukamilika Julia 20 mwaka huu.
“Kazi ya kutengeneza madawati
itakapokamilika Shule za Mkoa wa Iringa hazitakuwa na upungufutena wa madawqati
bali zitakuwa na ziadiyamadawati 850 na hiini kutokana na baadhi ya
Halkmashauri kuwa kutengeneza madawati ya zaidi na mengine
niyaleyaliyotolewakutoka Ofisi ya Mkoawa Iringa”alisema Masenza.
Masenza ambaye pia alitumia fursa
hiyo kuwashukuru wananchi na wadaumbalimbali wakiwamoawafanyakazi waliojitolea
kuchangia madawatihayo alisema hadikazihiyoinakamilika jumla ya Sh 50.4milioni
zimetumika kutengeneza madawati hayo.
“Nitumie fursa hii kuwashukuru wadau
mbalimbali,wafanyakazi wa Halmashauri na wananchi wote walioona umuhimu
wa kuchangia upatikanaji wa madawati haya”alisema Masenza na kuongeza.
“Mchango wao umekuwa na umuhimu
katika kuwaandaa vijana wetu tunapoelekea Taifa lauchumi wa kati ifikapo mwaka
2030,michango yao ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa ziada hiyo,kwani mkoa umetoa
madawati 200 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na madawati 100 kwa
Halmashauri za Kilolo,Iringa,Mji Mafinga na Mufindi”alisema Masenza.
0 maoni:
Chapisha Maoni