Jeshi la Polisi kanda maalumu ya
Dar es salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mchezo huo wenye mvuto mkubwa kwa
washabiki wa Tanzania, nchi za Afrika mashariki na Afrika nzima kuchezwa
katika hali ya usalama.
Aidha tunaomba wananchi wasiwe
na shaka yoyote ya kiusalama na pia watupe ushirikiano wa kutoa taarifa
kwa jambo lolote watakaloliona kuwa linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa
amani kwa kipindi chote watakapokuwa nje au ndani ya uwanja. Kutakuwa na CCTV Camera ili kuhakikisha sehemu zote mageti ya kuingilia na kutokea na maeneo yote yanaonekana na kuweka kumbukumbu za matukio yote.
Pamoja na hayo wananchi wanatakiwa kuwa watulivu katika kushangilia mechi hiyo, na kuepuka kufanya mambo yafuatayo:
·
Kuingia na chupa za kimiminika cha aina yeyote,
Kuingia na silaha ya aina yoyote
· Kupaki magari ndani ya uwanja·
Kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziwaruhusu.
KAMANDA WA POLISI MKOA IALA
DAR ES SALAAM
0 maoni:
Chapisha Maoni