Jumatano, 29 Juni 2016

MATUKIO KATIKA PICHA JANA BUNGENI DODOMA

B1Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali ya Wabunge Leo Bungeni Mjini Dodoma kuhusu mpango wa Serikali wa kuimarisha Viwanda  vilivyopo hapa nchini na kujenga vipya katika Mikoa mbalimbali.
B2Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako akieleza juu ya mkakati wa Serikali kuimarisha vyuo vya Ufundi Stadi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Mjini Dodoma.
B3Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakiyembe akiteta jambo na Mbunge wa Korogwe Vijijini Mhe. Steven Ngonyani Bungeni Mjini Dodoma Leo.
B4Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango  akijibu hoja za wabunge kuhusu Muswada wa Marekebisha ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016 Leo Bungeni Mjini Dodoma.
B5Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akitoa ufafanuzi kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha miundombinu ya Barabara hapa Nchini.
B6Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akitoa ufafanuzi kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha miundombinu ya Barabara hapa Nchini.
B8Mbunge Viti Maalum Mhe. Martha Mlata akichangia hoja wakati wa uwasilishwaji wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016.
B7 Baadhi ya Wabunge wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa katikati) mara baada ya kupitishwa kwa muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.
(Picha zote na Frank Mvungi-Dodoma)

0 maoni:

Chapisha Maoni