Mbunge wa Jimbo la
Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile(Mb) ameyataka Mataifa
kushirikisha Mabunge katika kufanikisha mpango wa Usalama wa Afya
Duniani (Global Health Security Agenda).
Akizungumza kwenye mkutano wa
masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)
na kufanyika Jijini Bali, Indonesia,, Dkt Ndugulile alisema, “Mabunge
yanaweza kutoa mchango mkubwa sana kwenye utekelezaji wa Mpango wa
Usalama wa Afya Duniani kwa kusimamia Serikali na kuhakikisha hatua zote
muhimu zinatekelezwa; kutunga Sheria zitakazosimamia utekelezaji wa
mpango huu pamoja na kuhakikisha mpango huu unapata fedha za kutosha
kutoka kwenye Bajeti ya Serikali”.
Dkt Ndugulile alisema kuwa
muingiliano wa shughuli za kilimo, mifugo na shughuli nyingine za
kibinadamu zimesababisha baadhi ya magonjwa ya wanyama kuleta athari kwa
binadamu na pia usugu wa madawa ya aina ya antibiotiki. Hivyo, kuna
haja ya wadau wa sekta hizi kuwa na ushirikiano wa karibu chini ya
mpango wa “Afya Moja” (One Health).
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni
(CCM) Dkt Faustine Ndugulile (Mb) (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa
masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani
(WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia.
Alisema kuwaIli mpango wa “Afya
Moja” ufanikiwe in lazima maboresho yafanyike kwenye uratibu wa sekta
mbalimbali ndani ya nchi na pia kuandaa mpango wa pamoja wa udhibiti na
kushughulikia majanga.
Dkt Ndugulile aliyasema hayo
kwenye mkutano wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani unaofanyika mjini
Bali, Indonesia. Mkutano huu ulioanza tarehe 27 Juni unatarajia kuisha
tarehe 30 Juni.
Dkt Ndugulile mbali ya kuwa
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya
Mabunge Duniani (Inter Parliamentary Union) kuhusiana na masuala ya
UKIMWI, Afya ya Wanawake, Vijana na Watoto.
0 maoni:
Chapisha Maoni