Mchezo wa kirafiki katika ya wafanyakazi wa kituo cha redio cha E fm na wasanii wa Bongo Fleva uliofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe umemalizika kwa wafanyakazi wa E fm kuibuka na ushindi wa goli 4-3.
Katika mchezo huo, mchezaji bora wa mechi hiyo alikuwa ni staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba baada ya kuonyesha kiwango bora kwa dakika kadhaa za kipindi cha pili alichocheza lakini pia kuifungia Bongo Fleva goli la tatu.
Magoli ya Bongo Fleva katika mchezo huo yalifungwa na TID, H Baba na Ali Kiba ambaye aliingia katika kipindi cha pili.
Pamoja na mchezo huo pia kulikuwa na kitendo cha kufurahisha kutoka kwa mwanamuziki TID ambaye alikuwa akicheza nafasi ya ushambuliaji ya timu ya Bongo Fleva kwani katika kipindi cha kwanza wakati E fm wakiongoza kwa goli 3-1 alitoka uwanja kutokana na kuona hali ni ngumu.
Baada ya E fm kufunga goli la tatu TID alitoka nje akavua jezi na viatu na kumwachia kocha wake, Kalapina kisha kuondoka huku akiwanyoshea mikono ya kushangilia mashabiki wa soka waliofika katika kiwanja hicho kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo.
DSC_4278
DSC_4280
DSC_4294
DSC_4307
DSC_4314
DSC_4326
DSC_4340
DSC_4341
DSC_4350
DSC_4355
DSC_4357
DSC_4361
DSC_4365
DSC_4366
DSC_4370