Katika kuelekea kilele
cha Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN)
lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere
barabara ya Kilwa jijini Dar.
Makonda alifika katika banda
hilo na kupata nafasi ya kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa UN
kuhusu kazi ambazo zinafanywa na shirika hilo hapa nchini.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akitoa maelezo ya
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) alipotembea
banda la shirika hilo lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho
ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja
wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia kila mwananchi alipotembelea
banda la Umoja wa Mataifa lillilopo katika ukumbi wa Karume kwenye
Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDG’s)
yaliyobandikwa katika banda la UN na jinsi walivyojipanga katika
kuelimisha wananchi kuhusiana na malengo hayo kwenye Maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Umoja
wa Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
barabara ya Kilwa jijini Dar. Kulia ni Maafisa Habari wa Umoja wa
Mataifa, Hoyce Temu na Usia Nkhoma Ledama. RC Makonda amekuwa mgeni
kwanza mashuhuri kutembelea banda hilo na kutoa baraka zake kwenye
maonyesho hayo.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu katika picha ya pamoja huku
wakiwa na bango maalum linalowakilisha rangi za malengo 17 ya SDGs na
mmoja wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo kwenye
ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa
jijini Dar.
Afisa Habari wa kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na
waandishi wa habari kwa lengo la kuhamasisha wananchi kutembelea banda
hilo na kujifunza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu SDGs na kujua
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini.
0 maoni:
Chapisha Maoni