Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi
miwili kwa mkandarasi Chicco anaefanya upanuzi wa njia ya kuruka na
kutua ndege katika uwanja wa ndege wa dodoma kuhakikisha kuwa ujenzi huo
unakamilika.
Akizungumza
mara baada ya kukagua kazi ya upanuzi wa uwanja huo, Prof. Mbarawa
amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa ujenzi wa uwanja huo
unafanyika kwa kuzingatia viwango vilivyokubalika katika mkataba na
kuukabidhi kwa wakati.
“Hakikisheni
upanuzi huu unakamilika kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja
wa ndege wa Dodoma, hasa mkizingatia umuhimu wake kitaifa’, amesema
Prof. Mbarawa.
Naye
Mkandarasi anaejenga uwanja huo amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa
kuwa atahakikisha ujenzi wake unazingatia viwango na kuukabidhi katika
muda uliokubalika kimkataba.
Zaidi
ya shilingi bilioni 11.8 zinatarajiwa kutumia katika upanuzi huo na
hivyo kuwezesha ndege nyingi zaidi kutumia uwanja huo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi Kampuni ya Chico, anayefanya upanuzi wa njia ya
kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa ndege wa Dodoma.
Ujenzi
wa Barabara ya Kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa ndege wa Dodoma
ukiendelea. Ujenzi huo kwa kiwango cha lami unatarajiwa kukamilika
katika kipindi cha miezi miwili.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Miradi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania
(TAA) Eng. Mbila Mdemu (wa pili kulia), wakati alipokagua maendeleo ya
mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma.
Meneja
wa Miradi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mbila
Mdemu, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa, alipokagua maendeleo ya upanuzi wa Uwanja wa
Ndege wa Dodoma.
0 maoni:
Chapisha Maoni