Ijumaa, 10 Juni 2016

Uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga waiwezesha TBL Mwanza kujinyakulia tuzo ya Mackay

tuz1Mkurugenzi wa ufundi wa TBL Group, Gavin Van Wijk akiongea na waandishi wa habari na wafanyakazi wa TBL Mwanza wakati wa hafla a kukabidhi tuzo
tuz2Meneja Msaidizi wa TBL Mwanza,Gabriel Pitso,akiongea wakati wa hafla hiyo
tuz3Meneja Msaidizi wa TBL Mwanza,Gabriel Pitso,akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi wa ufundi Gavin Van Wijk
tuz4Baadhi ya waandishi wa habari katika hafla hiyo
tuz5Viongozi wa kiwanda cha Mwanza katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kupokea tuzo
………………………………………………………………………………………………………………………..
Kiwanda cha TBL Mwanza kilichopo chini ya TBL Group na kikiwa moja ya kiwanda kinachoshikilia rekodi ya  ubora katika viwanda vya SABMiller duniani kimeshinda tuzo kubwa ya Mackay kutokana na kufanya uzalishaji kwa kutumia pumba za mpunga.
Mackay ni tuzo kubwa ya SABMiller ya kumuenzi mmoja wa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Graham Mackay ambaye katika kipindi chake cha kuitumikia kampuni hiyo aliendeleza kwa kiasi kikubwa na alifariki miaka mitatu iliyopita ambapo kampuni imeanzisha tuzo yake kwa viwanda vyake ambavyo vinafanya uzalishaji unaoendana sambamba na malengo ya kampuni .
Malengo ya SABMiller ambayo baadhi yake yanashahabiana na malengo ya Umoja wa Mataifa yamelenga katika kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira na unaoleta mabadiliko kwa jamii kwa kuziwezesha kujikwamua kimapato.
Akiongea baada  ya kukabidhi tuzo hiyo kwa uongozi na wafanyakazi wa TBL Mwanza,Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Group, Gavin Van Wijk,amekipongeza kiwanda kwa kuendelea kungaa na kujinyakulia tuzo  mbalimbali kama hii ya Mackay.“Ushindani ulikuwa mkubwa na ulihusisha viwanda mbalimbali  lakini hatimaye mmefanikiwa kunyakua tuzo hii na kuweka rekodi ya kuwa kiwanda cha kwanza kuipata barani Afrika”.Alisema
Alitoa shukrani kwa wateja wote wanaoendelea kuiunga mkono kampuni kwa kununua bidhaa zake na kuongeza kuwa siku zote kampuni itahakikisha inaongeza  uzalishaji na kuingiza bidhaa bora sokoni ikiwemo kusaidia huduma mbalimbali zinazoleta mabadiliko kwenye jamii.
Akiongea juu ya tuzo hii katika hafla ya kuipokea iliyofanyika kiwandani Mwanza ,Meneja wa kiwanda hicho Gabriel Pitso, alisema kuwa kiwanda hicho ndicho cha kwanza kupata tuzo hii nchini na ushindi huu umetokana na kufanya uzalishaji unaozingatia utunzaji wa mazingira kwa kutumia mashine zinazotumia pumba za mpunga na mashudu ambao kitaalamu hujulikana kama Dry –De- Husking (DDH)  .
Alisema kampuni mama ya SABMiller ilifanya utafiti na baada ya utafiti huo iliamua kabla ya kuanzisha teknolojia  ya uzalishaji usiotumia mafuta  ya dizeli kwenye viwanda vyake vyote ianzie katika kiwanda cha Mwanza ambapo katika miaka ya kwanza ya majaribio mafanikio makubwa yamepatikana kutokana na kutumia teknolojia hii ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji na kupunguza uharibifu wa mazingira.
Mbali na kupunguza athari za uharibifu wa mazingira na gharama za uendeshaji teknolojia hii kwa kiasi kikubwa inasaidia kuongeza vipato kwa wakulima wa pamba na mchele  na wafanyabiashara wanaokusanya pumba kwa ajili ya kukiuzia kiwanda “Zamani pumba za mchele zilikuwa takataka lakini hivi sasa zimegeuka lulu kwa kuwa zina soko tunazitumia katika uzalishaji hivyo kuna wafanyabiashara wanapita maeneo mbalimbali wakizikusanya kwa ajili ya kutuuzia na huu ndio uwekezaji mzuri unaonufaisha jamii inayoishi jirani na maeneo ya kiwanda na  ni moja ya malengo yetu”.Alisema.

0 maoni:

Chapisha Maoni