Ijumaa, 10 Juni 2016

JAJI MKUU AFANYA ZIARA KIBAHA NA KIGAMBONI

index
Na Lydia Churi- MAHAKAMA YA TANZANIA
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman leo amefanya ziara ili kukagua miradi ya ujenzi wa Mahakama za Wilaya na Mwanzo zinazojengwa mjini Kibaha na Kigamboni.
Aidha, katika ziara hiyo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga alimweleza Jaji Mkuu kuwa Mahakama ya Tanzania imeamua kutumia Teknolojia ya kuongeza ufanisi kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu iitwayo Moladi.
Alisema kupitia Teknolojia hiyo, jengo huweza kukamilika ndani ya siku 45 mpaka 70 huku ikiokoa gharama za ujenzi kwa kati ya asilimia 40 na 45.
Alisema kutokana upungufu mkubwa wa Mahakama nchini Mahakama ya Tanzania iliunda timu iliyokishirikisha Chuo Kikuu cha Ardhi na Baraza la Ujenzi la Taifa (National Construction Council) ili kutafiti teknolojia itakayotumia muda mfupi na yenye gharama nafuu kujenga majengo ya Mahakama nchini. 
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, ujenzi unaoendelea sasa katika maeneo ya Kibaha, Kigamboni, Mkuranga, Bagamoyo, Kinyerezi, Kawe na Ilala ni sehemu ya utafiti wa teknolojia hiyo ili baadaye itumike kwenye ujenzi wa mahakama nyingine katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema Mahakama ina upungufu wa majengo katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kuna majengo 960 tu wakati mahitaji ni kuwa na majengo 3963 katika kila kata nchini. Aliongeza kuwa kupitia teknolojia hii mahakama itajenga majengo bora na mengi kwa kipindi kifupi.
Moladi ni teknolojia inayotumika kujenga nyumba bora kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu iliyoanzishwa nchini Afrika ya Kusini mwaka 1986 ambapo ukuta unaojengwa kwa kutumia teknolojia hii hukauka kwa siku moja ili kupisha hatua nyingine ya ujenzi kuendelea.eknolojia hii mahakama itajenga majengo bora na mengi kwa kipindi kifupi.
Moladi ni teknolojia inayotumika kujenga nyumba bora kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu iliyoanzishwa nchini Afrika ya Kusini mwaka 1986 ambapo ukuta unaojengwa kwa kutumia teknolojia hii hukauka kwa siku moja ili kupisha hatua nyingine ya ujenzi kuendelea.

0 maoni:

Chapisha Maoni