Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez akiendesha semina fupi kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) (hawapo
pichani) inayoendelea mjini Dodoma chuoni hapa.
Katika kuhakikisha kila Mtanzania
anapata elimu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo
yanatakiwa kumfikia mtu mmoja mmoja, ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini
(UN) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
mafunzo ambayo yataweza kuwajengea uwezo kuhusu mpango huo na jinsi
unavyoweza kubadili maisha yao.
Alisema katika mafunzo hayo wametoa
elimu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi zaidi ya
200 na hayo siyo mafunzo ya kwanza kwani wameshatoa mafunzo kama hayo
kwa wabunge wa Tanzania lakini pia wameshafanya mafunzo kama hayo jijini
Arusha ambapo yalihudhuriwa na vijana zaidi ya 200.
“Tunataka kila Mtanzania ajue kuhusu
Malengo ya Maendeleo Eendelevu (SDGs) tumeshatoa elimu sehemu nyingine
hii siyo ya kwanza na tutaendelea kwenda maeneo mengine kutoa elimu
zaidi na katika hilo ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini ipo imejipanga
kufanya hivyo,” alisema Bi. Temu.
Nae Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Willy Komba alisema mafunzo hayo
yamewajenga na kupata elimu ambayo walikuwa hawajaipata awali inayohusu
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na pia kueleza kutokana na umuhimu
wake watakaa kuangalia ni jinsi gani wataweka katika mtaala wa masomo
ili wanafunzi wajifunze kuhusu SDGs.
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM) wakisiliza kwa makini wakati semina fupi kuhusu Malengo 17
mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) iliyoendeshwa na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya
SDGs, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa semina fupi ilihusisha
wanafunzi wa UDOM inayoendelea mjini Dodoma.
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDOM wa
Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya habari na Mawasiliano, Lobezi Kulilo
akihoji kuhusiana elimu ya SDGs kuwafikia watu walio vijijini.
Mwanafunzi wa Digrii ya kwanza ya Sayansi ya Kompyuta UDOM, Traygod Lyimo akiuliza swali kwa wakufunzi kuhusiana na SDGs.
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakipitia vipeperushi mbalimbali vyenye
taarifa za kina kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs)
wakati wa semina fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja
wa Mataifa nchini.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez, akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wa UDOM
wakati wa semina fupi kuhusu Malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo
mjini Dodoma jana.
Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Willy Komba akitoa neno la shukrani kwa
Umoja wa Mataifa kwa kuwapatia mafunzo ya SDGs mara baada ya kumalizika
semina fupi kwa wanafunzi wa UDOM.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari wa
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), James Msofe, Mtaalamu wa Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa
masuala ya SDGs, Hoyce Temu na Mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDOM wa
Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya Upashanaji Habari, Lobezi Kulilo katika
picha kumbukumbu wakilishilia mabango ya SDGs.
Baadhi ya wanafunzi wa UDOM walioshiriki
semina fupi kuhusu SDGs iliyoandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa
chuoni hapo katika picha ya pamoja na vibao vyenye Malengo 17 ya
Maendeleo Endelevu.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDOM
mara baada ya kumalizika kwa semina kuhusu Malengo ya Dunia
iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja Mataifa mjini Dodoma jana.
0 maoni:
Chapisha Maoni