Mratibu wa show ya Lady
Jay Dee ya Naamka Tena Tour ya mjini Dodoma, Mh. Catherine Magige
akizungumza machache na kutambua uwepo wa Naibu Spika wa Bunge na
waheshimiwa wabunge wenzake katika viwanja vya Royal Village mjini humo.
(Picha zote na Zainul Mzige)
Malkia wa Bongo Flava, Lady Jay Dee katika ubora wake.
Mwanamuziki Lady Jay
Dee na The Band wakitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake
katika harakati za kuwafikia mashabiki wake wote nchini nzima kwa show
aliyoi' brand' kama Naamka Tena Tour.
Mkali wa R & B kwenye Band ya Lady Jay Dee, John Music akitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma.
Vijana watanashati wa bendi Lady Jay Dee wakitoa burudani kwa mashabiki wa Dodoma.
Hoyce Temu, Esther Bulaya, Shyrose Bhanji na Hamisi Kigwangalla wakipiga shwangwe kwa Lady Jay Dee alipokuwa jukwaani.
Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwenye viwanja vya
Royal Village ilipofanyika show ya mwanamuziki Lady Jay Dee mwishoni mwa
wiki mjini Dodoma.
Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Bunge la
Afrika Mashariki (EALA), Mh. Shyrose Bhanji kwenye show ya Lady Jay Dee
iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mh. Esther Bulaya akiserebuka na Hoyce Temu katika show ya Lady Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa juma mjini Dodoma.
Mh. Halima Mdee, Mh. Catherine Magige, Mh. Esther Bulaya pamoja na Hoyce Temu wakiserebuka.
Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kawe, Mh.
Halima Mdee walipokutana kwenye show ya Lady Jay Dee.
Mwanamuziki Lady Jay Dee na Band yake wakishambulia jukwaa.
Mashabiki wa Lady Jay Dee wakiserebuka kwa raha zao.
Pichani juu na chini
ni Umati wa wakazi wa mjini Dodoma eneo la VIP wakiwemo waheshemiwa
wabunge wakisakata muziki wa Lady Jay Dee.
Upendo waliounyesha watu wa Dodoma kwa mwanamuziki Lady Jay Dee.
Mh. Halima Mdee akipata Ukodak na wananchi wa Dodoma wanaomkubali.
Mh. Shyrose Bhanji na Hoyce Temu wakikumbatiana walipokutana kwenye show ya Lady Jay Dee mjini Dodoma.
Mh. Catherine Magige na Mariam Nnauye wakitoka jukwaani kumtunza Malkia wa Bongo Flava nchini, Lady Jay Dee.
Mh. Catherine Magige katika ubora wake.
Mheshimiwa Catherine Magige na Mariam Nnauye wakipozi kwa picha.
Lady Jay Dee akiwapa raha mashabiki wake na muziki wa Live.
Waheshimiwa wabunge Hamisi Kigwangalla na Bonnah Kaluwa wakisakata burudani katika ukumbi wa Roya Village mjini Dodoma.
Mama Ankal Michuzi (mwenye nguo nyekundu) akijumuika na mashabiki wa Lady Jay Dee kuzungusha mduara.
Katika mkusanyiko huu
kwa mbaaali anaonekana Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. Tulia Ackson akicheza kwaito eneo la VIP na mashabiki wa
Lady Jay Dee.
Kwaito likiendelea kunoga.
Mheshimiwa Catherine Magige ambaye ni rafiki na shabiki mkubwa wa Lady Jay Dee akicheza na kuimba kwa raha zake.
Dada Beatrice Mkiramweni na Didi Nafisa wakijimwaga kwenye dancing floor.
Mwanadada Hoyce Temu na mfanyakazi mwenzake Didi Nafisa wakionekana kuguswa na nyimbo za mwanamuziki Lady Jay Dee.
Waheshimiwa wabunge
akiwemo, Mh. Bonnah Kaluwa na Mh. Mboni Mhita pamoja wa wabunge wenzao
nao walikuwepo kwenye show ya Lady Jay Dee.
Kutoka kushoto ni Hoyce Temu, Mh. Shyrose Bhanji, Esther Bulaya pamoja na Didi Nafisa wa UN Tanzania.
Lady Jay Dee katika ubora wake.
Mwanamuziki Lady Jay
Dee akikonga nyoyo za mashabiki wake akiwemo mmoja wa waheshimiwa
wabunge ambaye alishindwa kuvumilia na kupanda jukwaani kucheza nae.
Beatrice Mkiramweni
kutoka ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (kushoto) akisisitiza
jambo kwa Afisa Habari wa Bunge, Bw. Owen Mwandumbya (katikati) wakati
wa show la Lady Jay Dee ya 'NaamkaTenaTour' mjini Dodoma ambapo amepanga
kuzunguka mikoa yote ya Tanzania. Kulia ni Mtalaamu wa Mawasiliano wa
Shirika la Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu.






0 maoni:
Chapisha Maoni