Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Ushirika (WKMU) sehemu ya mifugo, Dkt. Maria Mashingo (kushoto)
akipata maelezo kutoka kwa mfugaji wa mdogo wa ng'ombe wa maziwa mjini
Njombe Paul Kasunga alipotembelea banda hilo maonesho wakati wa kilele
cha maadhimisho ya wiki ya unywaji wa maziwa yaliyofanyika kitaifa
mkoani Njombe wiki iliyopita. (Picha na Friday Simbaya)
Ng'ombe wa maziwa aina ya Ayshire ambaye ana umri miaka mitano anauwezo wakutoa lita 22 ya maziwa kwa siku.
Small milk producer Wema Gilbert
Ngimbuchi (blind) of Ikuna Village Ikuna in Ward, Njombe district sings
before the Permanent Secretary in the Ministry of Agriculture, livestock
and Cooperatives (livestock section) Dr. Mary Mashingo (left) as a sign
of thankfulness after she was handed over a registration certificate as
a milk producer supplied by Tanzania Dairy Board (TDB) during the peak
week of drinking milk made nationally in Njombe region last week. The
Staff of the East Africa Dairy Development (EADD II) for their unity,
they performed an act of mercy by the presenting a cow to her (Wema
Ngimbuchi) worth Tsh. 1,000,000/=. (Photo by Friday Simbaya)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Ushirika (sehemu ya mifugo) Dkt. Maria Mashingo (kushoto) akipeana
mkono na mzalishaji mdogo wa ng'ombe wa maziwa Wema Gilbert Ngimbuchi
(mlemavu wa macho) wa Kijiji cha Ikuna Kata ya Ikuna, wilyani Njombe,
mkoani Njommbe baada ya kumkabidhi cheti cha usajili cha mzalishaji
mdogo wa maziwa kilichotolewa na Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) wakati wa
kilele cha maadhimisho ya wiki ya unywaji wa maziwa yaliyofanyika
kitaifa mkoani Njombe wiki iliyopita. Wafanyakazi wa Mradi wa
uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (EADD II) awamu ya pili kwa
umoja wao,walifanya tendo la huruma kwa kumzawadia mfuaji huyo mtamba
wa ng`ombe mwenye thamani ya Tsh. 1,000,000/=. (Picha na Friday Simbaya)
Permanent Secretary in the Ministry of
Agriculture, livestock and Cooperatives (livestock section) Dr. Mary
Mashingo (left) shakes hand with small milk producer Wema Gilbert
Ngimbuchi (blind) of Ikuna Village Ikuna in Ward, Njombe district, after
handed over a registration certificate as a milk producer supplied by
Tanzania Dairy Board (TDB) during the peak week of drinking milk made
nationally in Njombe region last week. The Staff of the East Africa
Dairy Development (EADD II) for their unity, they performed an act of
mercy by the presenting a cow to her (Wema Ngimbuchi)worth Tsh.
1,000,000/=. (Photo by Friday Simbaya)
Baadhi ya wafanyakazi wa Mradi wa
uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (EADD II) kutoka mikoa ya
Mbeya, Njombe na Iringa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka
kitovu (dairy hub) kutoka kikundi cha wafugaji wadogo Halmashauri ya
Njombe (WAWAHANJO) katika kijiji cha Ikando Rahel Mhema akiongea na
mwandishi wa habari nyumbani kwake katika Ikando wilaya Njombe mkoani
njombe.
Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka
kitovu (dairy hub) kutoka kikundi cha wafugaji wadogo Halmashauri ya
Njombe (WAWAHANJO) katika kijiji cha Ikando Rahel Mhema akionesha
marobota yako ya hei (majani ya Rhodes boma) katika sehemu kavu
iliyoezekwa kuzuia jua na mvua alipotembelewa na mwandishi wa habari
hivi karibuni. Mfugaji huyo alipata mafunzo ya dhana ya kutengeneza hei
kwa njia rahisi ya kufunga marobota ya hei kwa njia mkono kutoka Mradi
wa uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (EADD II) awamu wa pili
kwa kushirikana na Heifer International.
Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka
kikundi cha wafugaji wadogo cha mshikamano Efrahana Kidenya katika
kijiji cha Mhaji wilayani Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe akiwa katika
shamba la ekari moja la malisho la majani (hei) aina ya Rhodes boma.
Ndama aliyezaliwa kwa njia Uhimilishaji
Bustani ya mboga za majani (kitchen garden).
Mshauri mwandamizi wa biashara kutoka
EADD II mkoa wa Njombe Joseph Lyamuya (kulia) akiwa mfugaji kutoka
katika kijiji cha Mlevela kata ya Igima wilayani Wanging’ombe, Mkoa wa
Njombe.
Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa Catherine
Mlowe akiwa na mme wake kutoka katika kijiji cha Mlevela kata ya Igima
wilayani Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe akionesha sehemu ya kuhifadhia
mkojo wa ng’ombe kutoka banda la ng'ombe unayotumika kama mbolea kwenye
bustani ya mboga za majani (kitchen garden).
Mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa
afrika mashariki (EADD II) awamu ya pili umeinua kipato cha wafugaji wa
ng’ombe wa maziwa katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya kwa
kuwajengea uwezo wa kutumia fursa ya kukusanya maziwa kwa pamoja, kupata
mafunzo na huduma mbalimbali za ufugaji na biashara ya maziwa kupitia
vyama vya wafugaji.
Meneja wa mradi nchini Mark Tsoxo
aliwaambia mtandao wa KALI YA HABARI jana kuwa mradi huo umeweza kufanya
wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa kuwa na mahali pakukusanyia na
kuhifadhi maziwa kwa wingi (dairy hubs), upatikanaji wa huduma za kinga
na tiba ya mifugo, uboreshaji wa koosafu (breeding line) ya ng’ombe,
upatikanaji wa mbegu za malisho, vyakula vya ziada vya mifugo pamoja na
kutoa ushauri na huduma za ugani.
Tsoxo alisema kuwa EADD II itawawezesha
wafugaji kitaalamu kutumia teknolojia mpya na stadi za uzalishaji
malisho, kuwa na vyanzo mbadala vya vyakula bora vya mifugo, ukusanyaji,
upoozaji na usafirishaji wa maziwa.
Alisema kuwa mradi huu wa EADD II
utaweka kupaumbele katika kuuganisha nguvu ya pamoja ya wafugaji na
usawa wa kijinsia ili kuongeza tija kuwanufaisha walengwa katika kaya
zipato 136,000 katika Afrika Mashairiki na jamii kwa ujumla. Kwa
Tanzania mradi umelenga kunufaisha kaya 35,000.
Mradi huu unatekelezwa na ushirikiano
baina ya mashirika matano ya maendeleo. Mashirika hayo ni Heifer
International Tanzania (ushauri na huduma za ugani), Technoserve
(ushauri wa biashara na masoko), ICRAF (mazingira na malisho), African
Breeders Service (Uhimilishaji) na International Livestock Research
Institute (Masuala ya utafiti)
0 maoni:
Chapisha Maoni