Ijumaa, 10 Juni 2016

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

ut6TAREHE 08.06.2016 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HADI SAA 15:00HRS KATIKA KISIWA CHA MAISOME KAMBI YA UVUVI MIGONGO KATA YA MAISOME TARAFA KAHUNDA  WILAYA SENGEREMA  MKOA WA MWANZA, KATIKA TUKIO LA KWANZA ASKARI WAKIWA DORIA  KATIKA KISIWA TAJWA HAPO JUU WAKIAMBATANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA SENGEREMA WALIFANIKIWA KUKAMATA NYAVU (KOKOLO) HARAMU ZA KUVULIA SAMAKI 17 NA TIMBA 81 AMBAYO NI MITEGO YA KIENYEJI YA KUTEGEA SAMAKI, VILIVYOTELEKEZWA NA WAVUVI WASIOJULIKANA  BAADA YA KUPATA TAARIFA ZA KUWEPO KWA ASKARI WANAOFANYA DORIA NA MISAKO KATIKA MAENEO YAO.
JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA MISAKO PAMOJA NA DORIA KATIKA KISIWA HICHO KWA KUHAKIKISHA WATUHUMIWA WALIOTELEKEZA NYAVU HIZO HARAMU WANAKAMATWA NA WENGINE WANAOSHIRIKIANA NAO PIA WANASAKWA ILI KUKOMESHA UVUVI HARAMU KATIKA KISIWA HICHO, HII NI BAADA YA KUPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA KISIWA TAJWA HAPO JUU KUNA WAVUVI AMBAO HUTUMIA ZANA HARAMU KATIKA SHUGHULI ZAO ZA UVUVI ZA KILA SIKU KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA TUKIO LINGINE SAWA NA TAREHE NA MAJIARA TAJWA  HAPO JUU KWENYE KISIWA CHA KASARAZI KATA YA BULYAHEKE TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA, ASKARI WAKIWA DORIA WALIFANIKIWA KUKAMATA NYAVU HARAMU ZA KUVULIA SAMAKI 9 NA TIMBA 04 ZILIZOTELEKEZWA NA WAVUVI WASIOJULIKANA  BAADA YA KUPOKEA TAARIFA YA UWEPO WA ASKARI WANAOFANYA DORIA KATIKA KISIWA HICHO. JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA UPELELEZI PAMOJA NA MSAKO WA KUWASAKA WAVUVI WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU ILI WAWEZE KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
BAADA YA ZANA HIZO HARAMU KUKAMATWA ZILITEKETEZWA KWA MOTO MBELE YA UONGOZI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WA WILAYA NA SERIKALI YA VIJIJI HIVYO NA WANANCHI WAKISHUHUDIA, HUKU MSAKO NA DORIA KATIKA VISIWA HIVYO NA VISIWA VINGINE VYA JIRANI BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWANI LIMEDHAMIRIA KUKOMESHA UHALIFU KATIKA MKOA WA MWANZA NA KUSIMAMIA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.

0 maoni:

Chapisha Maoni