……………………………………………………………………………………………………….
Na Atley Kuni- RS Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John
Mongella, ameiagiza taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi kuanza
kutumia visiwa na majabali makubwa yaliopo mkoani humo kwaajili ya
mazoezi ili kuweza kusaidia kupambambana na uhalifu ulioanza kujitokeza
katika siku za karibuni katika mkoa huo.
Akizungumza katika uzinduzi wa
maonesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo
hicho nchini Tanzania, Mongella amesema badala ya wakurufunzi hao
kwenda kufanya mazoezi kwenye maeneo ya nje ya mkoa ni vema kuanzia sasa
mkaanza kutumia visiwa vyetu,
“Ndani ya ziwa viktoria, hasa
huko visiwani kuna watu wanafanya uvuvi haramu sasa ni vema wakati wa
mazoezi mkawa mnafanyia kwenye maeneo hao ambayo yamekithiri kwa uvuvi
usio na tija”, alisema Mongella na kuongeza, “lakini sio kukomesha tuu,
uvuvi haramu bali pia itachagiza kwenye suala zima la utunzaji wa
mazingira na maliasili”
Amesema kuwa, endapo taasisi hiyo
ikitumia sehemu ya mafunzo kwa vitendo, kama mkoa utakuwa hauna haja
yakufunga shughuli za uvuvi kwa msimu na badala yake itasaidia kwenye
uzazi salama wa samaki na viumbe wengine wa majini.
Kwa upande wake mkuu wa chuo
hicho bi Lowael Damalu, amemuelezea mkuu wa mkoa kuwa chuo hicho hivi
sasa, kinauwezo wakudahili wakurufunzi 415 kwa msimu mmoja, ambalo ni
ongezeko kubwa ikilinganishwa na wakurufunzi 50, waliokuwa wakidahiliwa
na chuo hicho wakati kinaanza mwaka 1966, amesema mafanikio mengine
yaliyopatikana ni pamoja na kupata ithibati ya kutoka baraza la Elimu ya
ufundi, ongezeko la kozi za askari kuwa (basic technician, Law
Enforcement, uboreshaji wa maslahi ya watumishi, mafanikio mengine
ameyataja kuwa ni kuongezeka kwa miundombinu na vifaa vya kufundishia,
lakini pia taasisi kuwa na tovuti yake ya www.pasiansiwildlife.ac.tz sambamba na taasisi kujipatia ardhi.
Mkuu huyo wa chuo amesema mbali
yakuwa na mafanikio chuo hicho bado kinakabiliwa na matatizo ya uchakavu
wa baadhi ya mabweni, uchache wa nyumba za watumishi, vilevila
kutokuwepo kwa sheria ya uanzishwaji wa taasisi sambamba na uhaba wa
ajira kwa wakurufunzi wanao hitimu katika chuo hicho.






0 maoni:
Chapisha Maoni