Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) akimkabidhi Mbwana Samatta
(kushoto) zawadi ya kitabu kinachozungumza utalii wa Tanzania na
Tanzania kwa ujumla.
Mbwana
Samatta (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo baina yake na
Menejimenti ya Bodi ya Utalii Tanzania katika ofisi za Bodi hiyo jijini
Dar es salaam leo.
Mbwana
Samatta (katikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya
TTB wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi hiyo Bi Devota Mdachi.
……………………………………………………………………………………………
Na: Geofrey Tengeneza
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania
Mbwana Ally Samatta (23) anayecheza kandanda la kulipwa katika klabu
ya Genk nchini Ubelgiji amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
kuwa Balozi wa hiari wa Tanzania na kusaidia kuitangaza Tanzania kama
eneo la Utalii nchini Ubelgiji na Ulaya kwa ujumla.
Samatta ametoa ahadi hiyo leo
alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii jijini Dar es salaam na kuwa na
mazungumzo na Menejimenti ya Bodi hiyo kuhusu kumtumia katika kutangaza
vivutio vya utalii na Tanzania kimataifa.
“ Kama mtanzania ninawiwa kwa
nchi yangu hivyo nina furaha na niko tayari kitangaza nchi yangu kama
eneo la utalii popote nitakapokuwa” alisema. Aliongeza kwamba nchi
nyingi duniani hutumia watu wao maarufu ikiwa ni pamoja na wachezaji wa
kimataifa kuzitangaza nchi zao.Ameipongeza Bodi TTB kwa mkakati wa
kuwatumia watanzania mbalimbali maarufu katika kuitangaza Tanzania
akaahidi kufanya kila litakalowezekana ikiwemo kutumia mitandao yake ya
kijamii kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota mdachi amedokeza kuwa
TTB itatazama namna nzuri kabisa ya kumtumia Mbwana Samatta kutangaza
utalii wa Tanzania na Tanzania kwa ujumla kama eneo zuri kwa utalii.
Mbwana Samatta amesaini mkataba
wa kuichezea klabu ya Genk ya Ubelgiji utakaomalizika mwaka 2020.
Sammata ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa star,
alitwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya
Afrika.
0 maoni:
Chapisha Maoni