Kaimu
Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme,Mhandisi Leornard Masanja(
wa pili kulia) akikagua baadhi ya trasfoma zilizobiwa mafuta katika
ofisi ya Tanesco wilayani Bagamoyo, kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa
Pwani, Mhandisi Martin Madulu na Meneja Tanesco Wilaya ya Bagamoyo (
kushoto )
Baadhi ya transfoma zilizoibwa mafuta zikiwa katika ofisi ya Tanesco Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kaimu
Kamishna wa Nishati anayeshughulikia umeme,Mhandisi Leornard Masanja(
wa pili kulia) akikagua baadhi ya trasfoma zilizobiwa mafuta katika
ofisi ya Tanesco wilayani Bagamoyo, kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa
Pwani, Mhandisi Martin Madulu na Meneja Tanesco Wilaya ya Bagamoyo (
kushoto )
………………………………………………………………………………………………………………..
Na Zuena Msuya, Bagamoyo Pwani
Wizara ya Nishati na Madini
imesema itaendelea kuimarisha miundombuni ya upatikanaji wa huduma ya
umeme wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ili kuondoa malalamiko ya mara kwa
mara yanayotolewa na wateja.
Kaimu Kamishna wa Nishati
anayeshughulikia umeme, Mhandisi Leornard Masanja alisema hayo wilayani
Bagamoyo baada ya kufanya ziara katika Ofisi ya shirika la umeme nchini
(Tanesco) hivi karibuni.
Akiwa katika ziara hiyo,
Mhandisi Masanja alielezwa kuwa transfoma 56 ziliibwa mafuta na
kusababisha wananchi wengi kulalamikia Tanesco kwa kuchelewa kuwapatia
huduma ya umeme licha ya kukamilisha hatua zote za kuunganishwa na
huduma hiyo na umeme kukatika mara kwa mara.
Pia alielezwa kuwa, Tanesco
imekuwa ikichelewa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo
hayo pindi inapotokea hitilafu ya umeme au kukatika kwa huduma ya umeme
katika eneo fulani la Wilaya na Mkoa huo.
Baada ya kupokea malalamiko hayo,
Mhandisi Masanja aliwataka Meneja Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi
Martin Madulu pamoja na Meneja wa Wilaya ya Tanesco wa Wilaya ya
Bagamoyo, Mhandisi Julius Doyi kutoa ufafanizi wa namna ya kukabiliana
na changamoto hizo pamoja na kutatua malalamiko hayo kutoka kwa Meneja
Tanesco, Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu pamoja na Meneja wa Wilaya
ya Tanesco Wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi Julius Doyi.
Kwa upande wake Meneja Tanesco,
Mkoa wa Pwani Mhandisi Martin Madulu, alisema kuwa malalamiko hayo
yanatokana na uchache wa miundombinu hasa kwa wale wanaohitaji
kuunganishiwa huduma ya umeme.
Aidha alifafanua kuwa watumishi
wachache waliofukuzwa wamekuwa wakidaiwa kuhujumu shughuli nzima za
kuunganisha huduma za umeme kwa wananchi kwa kudai rushwa kwanza jambo
lililokuwa likiwakatisha tamaa wananchi.
Hata hivyo alielezwa kuwa, tayari
wafanyakazi wanane wamefukuzwa kazi wilayani bagamoyo kwa makosa
mbalimbali ikiwemo rushwa,matumizi mabaya ya ofisi na kuchelewesha
huduma kwa wananchi.
Naye Meneja wa Tanesco wilayani
Pwani Mhandisi Julias Doyi alisema kuwa tatizo la kuchelewa kuwahudumia
wananchi hasa wale wanaopata tatizo la kukatika huduma ya umeme
linatokana na miundombinu mibovu ya kuwafikia wananchi hao na kuwa na
Gari moja la kutoa huduma kwa wilaya nzima.
Aliongeza kuwa Tanesco wamekuwa
wakichelewa kupata taarifa kutoka kwa wananchi kutokana na wengi wao
kutoa taarifa hizo kupitia Viongozi wa Serikali za mitaa na kusababisha
taarifa hizo kuchelewa kuwafikia Tanesco.
0 maoni:
Chapisha Maoni