Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha mashauriano ya pamoja baina ya Serikali na
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuhusu adhma ya ujenzi wa viwanda nchini
wakifuatilia kwa makini kikao hicho kilichoitishwa na Serikali kupitia
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji pamoja Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na
Ulemavu). Kikao hicho kilifanyika leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF), Bw. Adam Mayingu
na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Bw.
William Urio wakifuatilia kikao cha pamoja baina ya mifuko ya hifadhi
ya jamii na Serikali kuhusu adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa
uchumi unaotegemea viwanda.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF), Bw. Adam Mayingu
na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), Bw.
William Urio wakifuatilia kikao cha pamoja baina ya mifuko ya hifadhi
ya jamii na Serikali kuhusu adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa
uchumi unaotegemea viwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Godius Kahyarara (katikati)
akizungumza katika kikao baina ya mifuho ya hifadhi ya jamii na Serikali kilichozungumzia
adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Urio na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO.
akizungumza katika kikao baina ya mifuho ya hifadhi ya jamii na Serikali kilichozungumzia
adhma ya utekelezaji wa agizo la ujenzi wa uchumi unaotegemea viwanda. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Urio na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO.
…………………………………………………………………………………………………………………….
Jonas Kamaleki Maelezo Dodoma
Serikali imekubaliana na mifuko
ya hifadhi ya jamii kuanza utekelezaji wa ujenzi wa viwanda nchini ili
kuhakikisha kuwa adhma ya Tanzania ya kufikia uchumi wa viwanda
inafanikiwa ifikapo mwaka 2020.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli aliyeitaka mifuko hiyo kuwekeza katika ujenzi wa viwanda nchini.
Akizungumza mara baada ya kikao
cha pamoja baina ya Serikali na mifuko hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Ulemavu, Jenister
Mhagama alisema Serikali imekusudia kuhakikisha uanzishwaji wa viwanda
unaanza haraka na kuongeza fursa za ajira nchini.
Mhagama alisema kuwa mali ghafi
na nguvu kazi ya kutosha zipo hapa nchini hivyo hakuna sababu ya
kuchelewa kuanza, ambapo Serikali imepanga hadi kufikia mwishoni mwa
mwaka 2016, utekelezaji wa adhma hiyo inaanza kuonekana machoni mwa
Watanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya hifadhi ya Jamii
(SSRA)alisema, Irene Isaka alisema ni agizo hilo limekuja katika wakati
mwafaka kwa kuzingatia kuwa kwa mifuko ya Hifadhi ya jamii imekusudia
kutekeleza kwa vitendo adhma ya Serikali ya awamu ya tano inayosisitiza
kuijenga Tanzania kupitia uchumi wa viwanda.
Kwa mujibu wa Isaka alisema
kuwa kanuni na mifumo ya mifuko hiyo inaruhusu suala la uwekezaji katika
viwanda ama kwa njia ya ubia au ya hati fungani au kutoa mikopo kwa
wanotaka kuwekeza katika viwanda.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt, Adelhelm Meru alisema uwekezaji
katika viwanda ni suala ambalo linawashirikisha wadau wengi zikiwemo
wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya malighafi za viwandani,
Elimu kwa ajili ya ujuzi wa watu wa kufanya kazi viwandani na Wizara ya
Nishati na Madini kwa ajili ya nishati ya kuendesha viwanda.
“Kwa kuangalia raslimali tulizo
nazo tumewaomba wadau waanze na viwanda ambavyo vilikuwepo lakini kwa
sasa havifanyi kazi kama vile Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC),
General Tyre, NARCO na Kiwanda cha Viwadudu cha Kibaha, alisema Dr.
Meru na kuongeza kuwa malighafi za viwanda hivi zinapatikana hapa
nchini.
0 maoni:
Chapisha Maoni