Takriban
maafisa 302 wa polisi wamefutwa kazi nchini Kenya kwa kukataa kukaguliwa
tangu mpango huo wa kutaka kukabiliana na ufisadi kuanzishwa mwaka
2013,kulingana na tume inayotekeleza ukaguzi huo.
Hayo
yalibainishwa na Jonhston Kavuludi ,anayeongoza tume hiyo ya huduma za
maafisa wa polisi huku maafisa wa polisi wakijiandaa kuhojiwa na jopo
katika mji wa magharibi wa Kisumu.
Ukaguzi
huo ni mpango wa uma na hufanywa mbele ya kamera ambapo maafisa uhojiwa
kuhusu mali na fedha wanazomiliki huku mgongano wowote wa maslahi
ukichunguzwa.
Mwezi
uliopita wakati jopo hilo lilipokuwa Mombasa ,afisa mmoja wa idara ya
trafiki hakuweza kusema ni wapi alipata takriban dola 500,000 ambazo
ziliwekwa katika mtandao wa simu unaotuma fedha ama kupokea na akaunti
yake ya benki.
Wakenya
katika mitandao ya kijamii walishangazwa na kuelezea vile
wanavyolazimishwa kutoa hongo baada ya kukamatwa kwa makosa ya trafiki.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni