Mwanzilishi
wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, amezindua kampeni ya kusaidia watu
maskini zaidi barani Afrika, kusini mwa jangwa la sahara, kwa kufuga
kuku
Bilionea huyo Bill Gates anasema kuwa kufuga kuku kunaweza kuwa kifaa muhimu katika kukabiliana na ufukara hohe hahe.
Ameahidi kutoa kuku 100,000, na ukurasa katika mtandao wa mradi huo tayari umewavutia na kusambazwa kwa maelfu ya watu.
Umoja wa
Mataifa unakisia kuwa asilimia 41 ya watu katika Bara la Afrika, Kusini
mwa jangwa la Sahara wanaishi katika ufukara mkubwa.
Bwana
Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata zaidi ya
Dola 1,000 kwa mwaka. Mtu hutajwa kuwa maskini iwapo anapata Dola 700
pekee kwa mwaka.
Alisema
kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia zaidi ya asilimia 30 ya watu
wanaoshi mashambani Kusini mwa Jangwa la Sahara ili wapate huduma ya
kufuga kuku wa hali ya juu mbao watachanjwa. Alisema hatua hiyo
itaongeza watu wanaofuga kuku kwa asilimia tano.
Ananukuliwa
akisema kuwa kuku huongezeka maradufu na kwa hivyo hakuna uekezaji ulio
na mapato mazuri kwa asilimia ya juu kuliko ufugaji kuku.
Alisema
hayo alipokuwa akianzisha mradi huo jijini New York. Anashirikiana na
shirika na kutoa misaada kwa maskini la Heifer International.
Watu milioni 800 huishi katika hali ya umaskini hohehahe, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni