Jumanne, 14 Juni 2016

ZAIDI YA WAKAZI 4000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI PANGANI

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh MartineShigella katikati akipata maelezo ya mradi wa maji Boza-Kimang’a kutoka kwa Mhandisi wa Maji Wilaya ya Pangani,Mohamed Seif wakati alipofanya ziara wilayani humo kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya
Pangani,Esteria Kilasi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martine Shigella mwenye suti katikati akitazama mradi wa Maji  wa Boza-Kimang’a wa kwanza kushoto ni Mhandisi wa Maji Wilaya ya Pangani,Mohamed Seif na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Ahmed
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martine Shigella mwenye suti akiingia kwenye tanki la kuhifadhia maji

ZAIDI ya wakazi 4009 wa Kijiji cha Boza Kimang’a wilayani Pangani Mkoani
Tanga watanufaika na mradi wa huduma ya maji kupitia program ya maji na
usafi wa mazingira vijijini (NRWSSP) katika mpango wa vijiji vya
nyongeza.
Hayo yalisemwa juzi na Mhandisi wa Maji wilaya ya Pangani, Mohamed Seif
wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji Boza-Kimang’a kwa Mkuu
wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliyefanya ziara ya kukagua na
kuzindua miradi ya maendeleo.
Alisema kuwahadi sasa kisima kirefu kimekwisha kuchimbwa na usanifu wa
mradi huo umefanyika na mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa
miundombinu ya kusambaza maji Saxon Building Contractor na kusimamiwa na
Mtaalamu mshauri Don Consult Limited.
Mhandisi huyo alisema mradi huo ambao umeanza February 19 mwaka huu na
kutarajiwa kukamilika Novemba 19 ukigharimu kiasi cha sh.milioni 884.4
ambapo shughuli zitakazofanyika ni uchimbaji wa kisima kirefu,ujenzi wa
nyumba ya kuhifadhia mashine,ujenzi wa matenki mawili ya kuhifadhia
maji.
Aliongeza kazi nyengine ni ujenzi wa vituo 16 vya kuchotea
maji,kununua na kufunga mashine za kusukuma maji,kununua na kufunga
mabomba ya viungio ikiwemo kuvuta umeme kwenye eneo hilo la mradi.
Akizungumza wakati akizundua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine
Shigella aliwataka wananchi kuhakikisha  wanautunza vema ili uweze
kuwasaidia wao na vizazi vijavyo ikiwemo kuacha kuharibu vyanzo vya
maji.
Picha na stori kwa Hisani ya Blog
ya Kijamii ya Tanga Raha.

0 maoni:

Chapisha Maoni