Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akizungumza wakati wa
kukabidhi Madawati 50 yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi kwa
shule ya msingi Mnazi katika manispaa ya Moshi ikiwa ni kuunga mkono
agizo la rais John Magufuli la kupunguza tatizo la Madawati kwa shule za
msingi.
Meneja
wa benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungungumza juu ya
hatua ya benki hiyo kuunga mkono agizo la rais John Magufuli la kutatua
tatizo la Madawati kwa shule za msingi nchini.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika hafla hiyo ya
kukabidhi Madawati 50 yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi kwa
shule ya msingi Mnazi.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakifuatilia hafla hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Deodatus Nyoni
akizungumzia juu ya upungufu wa Madawati 701 ulipo sasa kwa shule za
msingi na Sekondari.
Meneja
wa benki ya Azania tawi la Moshi, Hajira Mmambe akimkabidhi mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky Madawati yaliyotolewa na benki
hiyo. Wengine ni wanafunzi wa shule ya msingi Mnazi.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadicky (katikati) akiwa ameketi
kwenye moja ya Madawati yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi
kwa shule ya msingi Mnazi, kulia ni mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus
Makunga na kushoto ni meneja wa Azania benki tawi la Moshi, Hajira
Mmambe.
Wanafunzi katika shule ya msingi Mnazi wakiwa wamekaa katika Madawati yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadicky, akisalimiana na wanafunzi katika shule hiyo.
Mstahiki
Meya wa manispaa ya Moshi, Raymond Mboya akitoa neno la shukrani mara
baada ya kupata msaada wa Madawati kutoka Benki ya Azania tawi la
Moshi.
Mstahiki
Meya wa manispaa ya Moshi, Raymond Mboya akiteta jambo na Meneja wa
benki ya Azania tawi la Moshi, Hajira Mmambe wakati wa hafla ya
kukabidhi wa Madawati kwa shule ya msingi Mnazi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadicky akisalimiana na wafanyakazi
wa benki ya Azania tawi la Moshi pamoja na watumishi wa halmashauri ya
Manispaa ya Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog kanda ya kaskazini.
0 maoni:
Chapisha Maoni