Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert
Richard akimuonyesha ramani inayoonyesha maeneo ambayo mfuko umetekeleza
miradi ya kupeleka huduma za mawasiliano baadhi ya wa wananchi
waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO leo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert
Richard akiwaelezea jambo baadhi ya wa wananchi wa Dar es salaam
waliotembelea banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO .
Mwanasheria
wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Ambokile Mwakaje (Kulia)
akimuelekeza baadhi ya maeneo walipotekeleza miradi ya huduma za
mawasiliano mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la mfuko huo katika
maonyesho ya SIMU EXPO.
Afisa
Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Edwin Makala
akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea banda la
mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert
Richard akiwaelezea jambo baadhi ya wa es Salaam wananchi waliotembelea
banda la mfuko huo katika maonyesho ya SIMU EXPO.
Baadhi
ya wananchi wakiwa katika banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
(UCSAF) wakati wa maonyesho ya SIMU EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija,MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija,MAELEZO
Zaidi ya dola za kimarekani
milioni 36 zimetumika katika kufikisha huduma za mawasiliano ya simu
katika maeneo ya vijijini yasiyo na mvuto wa kibiashara nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa
Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert
Richard wakati wa maonyesho ya SIMU EXPO 2016 leo jijini Dar es Salaam.
Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
unashiriki maonyesho hayo ili kutoa elimu kwa umma juu ya shughuli
mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
Albert amesema kuwa kazi kubwa ya
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ni kufikisha huduma za mawasiliano ya
simu katika maeneo yote ya vijini yasiyo na mvuto wa kibiashara ambapo
makampuni ya simu yanasuasua kupeleka huduma hiyo.
“Sisi kama Taasisi ya Serikali
kazi yetu kubwa ni kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo yote ya
vijini ambayo makampuni binafsi yanasuasua kupeleka huduma kutokana na
msukumo wa kibiashara.” Alisema Albert.
Aliongeza kuwa mradi wa kwanza
uliotekelezwa na mfuko huo umegharimu takribani Dola za Kimarekani
milioni 5.8 ambapo jumla ya Kata 52 zimenufaika na mradi huu kwa
kuunganishwa na huduma za mawasiliano ya simuK.
Pamoja na jitihada za Serikali
kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma za mawasiliano ya simu
kumekuwa na changamoto katika kutekeleza azma hiyo kwa wakati kutokana
na ufinyi wa bajeti na kukosekana kwa miundombinu rafiki kama vile
Barabara na Umeme.
Kutokana na changamaoto hizo
Albert ametoa rai kwa jamii kuwa na subira wakati utekelezaji wa miradi
ya kupeleka huduma za mawasiliano ya simu katika maeneo yao ukiendela
hatua kwa hatua kadri fedha zinavyopatikana.
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
(UCSAF) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2006 kwa lengo la
kupeleka na kufanikisha mmawasiliano kwa wananchi waishio katika maeneo
machache ya mijini na maeneo mengi ya vijijini yasiyo na mvuto wa
kibiashara kwa watoa huduma ya mawasiliano.
0 maoni:
Chapisha Maoni