…………………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
SAKATA la mgogoro wa ardhi kwa
wananchi wa kijiji cha mwavi kata ya Fukayosi kilichopo Wilayani
Bagamoyo Mkoani Pwani na mwekezaji ambaye ni mkorea limechukua sura mpya
baada ya mkuu wa Wilaya hiyo kuamua kuliingilia kati suala hilo kwa
lego la kurudisha hali ya amani na utulivu pamoja na kumaliza tofauti
zilizokuwepo.
Mgogoro huo ambao umeonekana
kuwa na mvutano mkubwa kutokana na mwekezaji huyo kupatiwa eneo lenye
ukumbwa wa hekari 231 za serikali ya kijiji pasipo kuwashirikisha
wananchi wenyewe kitu ambacho kilichangia kwa kiasi kikubwa kutoelewana
kati ya wanakijiji na mwekezaji huyo.
Akizungumzia kuhusina na sakata
hilo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema kwamba baada ya
kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao aliamua kufanya uchunguzi wa
kina na kubaini mwekezaji huyo alipewa eneo hilo kwa ajili ya
uwekezaji,ambapo kwa sasa wamekubaliana naye hekari 131 zirudishwe kwa
wananchi wenyewe na yeye abakiwe na hekari 100 tu.
“Jamani wananchi wa kijiji cha
mwavi mimi baada ya kuniletea malalamiko hayo nimeyafanyia kazi kwa
kina kabisa ambapo nimekutana na mwekezaji huyo tumeongea naye juu ya
suala hilo na amekubali kuzirudisha hekari 131za ardhi kwa wananchi
nayeye atabakiwa na hekari 100 kwa ajili uwekezaji katika eneo hilo
ambapo atajenga kituo cha kilimo, shule, zahanati pamoja na mambo
mengine hivyo tuwe watulivu tumwone kama ataziendeleza kama
tulivyokubaliana.
Alisema kwamba serikali ya
awamu ya tano ambayo inangozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli
itahakikisha kwamba inaleta mabadiliko chanya kwa kuzingatia usawa bila
ya kuwa na uonevu wowote ule hasa katika masuala ya ardhi ambayo
yameonekana kuwa ni changamoto kubwa katika Wilaya ya bagamoyo na maeneo
mengine, na kuahidi kushirikiana nao mambo yote ya kimaendeleo.
Aidha amepiga marufuku kwa
wenyekiti wa vijiji na vitongoji vyote kutouza ardhi kiholela bila ya
kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na badala yake tabia hiyo
waiche mara moja vinginevyo atawachukulia hataua kali za kisheri ili iwe
fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
“Hii tabia ya watendaji wetu
kufanya jambo la kuuza ardhi bila kuzingatia sheria ni baya sana na ndio
maana linatufukisha katika hatua kama hii ya kugombania ardhi na
kusababisha migogoro sasa sitaki kuona hali hiyo, kwani huna mamlaka
yoyote ya kuuza ardhi hata mita mbili kwa hiyo naomba hili lizingatiwe
sitaki kuona migogoro ya ardhi katika Wilaya ya Bagamoyo, alisema
Mwanga.
Kwa upande wao wananchi wa
kijiji hicho akiwemo Ramadhani Mfaume,Salum Hamad,Kulwa Ramadhani pamoja
na Semeni Manga wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo
wamesema kwamba walikuwa wanashindwa kufanya shughuli zozote za
kimaendeleo kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo wa ardhi baina yao na
mwekezaji huyo.
Walisema kwamba mwekezaji huyo
alipewa eneo hilo tangu mwaka 1997 na baadhi ya watendaji wa kijiji kwa
ajili ya uwekezaji lakini wanashangaa ameshindwa kuliendeleza kitu
ambacho waliamua kwenda kutoa kilio chao kwa mkuu wa Wilaya kuhusiana na
hekali hizo ambapo wanashukuru ameweza kulishughulikia suala hilo na
kufanikiwa kuzirudisha hekari 131 za kijiji.
“Kwa weli sisi kama wananchi wa
kijiji cha mwavi tulikuwa katika hali ya mvutano mkubwa wa siku nyine
na mwekezaji huyo ambaye ni mkorea, juu ya kutuchukulia ardhi yetu
lakini tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mkuu wetu wa Wilaya
kuweza kulitatua suala hilo ambalo lilikuwa inatumbumbua kwa muda mrefu,
walisema wanakijiji hao.
Pia waliongeza kuwa kurudishwa
kwa hekari hizo 131 zitaweza kuwapa fursa ya kuweza kufanya shughuli
mbali za kimaendeleo ikiwemo kujenga ujenzi wa shule kwa ajili ya watoto
wao,masoko, pamoja na zahanati kwani hapo awali walikuwa hawana huduma
za karibu katika kijiji hicho.
Pia mwandishi wa habari hizi
iliweza kupata fursa ya kuzungumza na mmwekezaji huyo ambaye ni Mkorea
anayejulikana kwa jina la Yum Yun Hwa ambapo alisema kwamba lengo lake
kubwa la kuchukua eneo hilo ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa eneo
hilo kwa kuweka viwanda, shule, zahanati pamoja na kuanzsiha kituo
maalumu cha kilimo.
Yum hwa alibainisha kwamba
katika kuunga juhudi za serikali ya Tanzania katika kuendeeza kilimo cha
kisasa amepanga kuwaleta wataalamu kutoka nchini korea ambapo watakuja
katika kituo hicho kwa ajili ya kufundisha masuala mbali mbali ya
kilimo, na kuongeza kuwa tayari wameshafanya ununuzi wa vifaa ikiwemo
matrekta,Power tila ambayo yatakuwa kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Kijiji hicho cha mwavi
kilichopo kata ya Fukayosi Wilayani Bagamoyo kiliingia katika mgogoro wa
ardhi na mwekezaji huyo tangu mwaka 1997, ambapo kutokana na juhudi
zilizofanywa na Mkuu wa Wiaya ya Bgamoyo kuamua kuingilia katia sakata
hili kumeweza kusaidia kutokana na mwekezaji huyo kukubali kuwarudhishia
ardhi yao wananchi yenye ukumbwa wa hekari 131.






0 maoni:
Chapisha Maoni