Polisi nchini
Burundi inawashikilia kundi kubwa la wanafunzi wa sekondari kwa kosa la
kuharibu picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza.
Waangalizi wanasema maafisa wa serikali walianza kupambana na kile kinachoonekana kuongezeka kwa visa vya kuharibu picha ya rais katika vitabu vya wanafunzi shuleni.
Mwezi uliopita, zaidi ya wanafunzi mia tatu walitimuliwa shuleni katika mji wa Ruziba baada ya walimu kukuta vitabu vyenye picha ya rais vimeharibiwa kuandikwa ujumbe wa matusi.
Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikiwa masuala ya watoto UNICEF limelaani kukamatwa na kufukuzwa kwa watotot hao, na kusema shule zinatakiwa kuheshimiwa kama maeneo salama kwa watoto.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi nchini Burundi tangu rais Nkurunziza kuamua kuwania muhula wa tatu kinyume cha katiba ya nchi hiyo hapo mnamo mwaka jana.
Zaidi ya watu mia nne na hamsini wameuawa.
BBC.
0 maoni:
Chapisha Maoni