Wanafunzi wametakiwa kuwa waadilifu pindi wanapomaliza chuo na kwenda kuingia makazini.
Kauli hiyo ameitoa Mwenyekiti wa
bodi ya Ushauri TAREA, Godwin Msigwa (pichani) ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu
Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend
iliyopita.
Msingwa alisema ni vyema vijana
wakatambua kuwa maisha mazuri ni yake ya kufanya kazi kwa uadilifu na
kuacha ujanja ujanja katika kazi.
“Leo mnaenda mtaani mtapata kazi
ninawaomba mkafanye kazi kwa uadilifu, mfano wewe ukipata kazi ya
kusimamia manunuzi ya dawa muendele ukanunue dawa zenye ubora maana
usipofaya hivyo utasababisha vifo vya watu na hiyo dhambi si ndogo,
Muogopeni Mungu,’ Alisema Msigwa.
Aliongeza kuwa wakati umefika kwa
watanzania wakaonyesha uzalendo kwa mambo yao wenyewe, wasingoje mpaka
wasukumwe katika kufanya kazi kwa bidii.
Mchungaji wa KKKT akitoa neno
wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu
Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend
iliyopita.
Wahitimu wakifuatilia neno kutoka
kwa mchungaji wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa
vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)
yaliyofanyika weekend iliyopita.
Katika neno alililolitoa mchungaji huyu aliwaasa wahitimu kuwa na hofu ya Mungu pindi wanapopewa majukumu ya kazi.
Mgeni rasmi mwenyekiti wa bodi ya
Ushauri TAREA, Godwin Msigwa (wa tatu toka kushoto) akiserebuka na
mchungaji wa KKKT pamoja na wageni waalikwa.
Wahitimu wakijimwaga.
Mchungani akiwaombea wanafunzi
wakafanye vyema katika mitihani yao wakati wa mahafali ya umoja wa
wanafunzi wa kikristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita.
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
0 maoni:
Chapisha Maoni