Mtaalamu
wa kujitolea kutoka nchini Japan, Bi.Yuka ITO, akielezea namna
alivyofanya kazi katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa
hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan
waliomaliza muda wao. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi mapema leo.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto)
akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw.
Kosuke MATSUDA aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini katika
hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi mapema leo.
Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba ( wa tatu kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka
nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla
fupi ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine ni watumishi wa
Ofisi ya Rais-Utumishi na wawakilishi kutoka JICA.
Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba (kulia) akifuatilia
maelezo ya Bi. Yuka ITO ya namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya
Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa
kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi
wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.
0 maoni:
Chapisha Maoni