Wafanya
kazi wa Jumuia ya Muzdalifat wakitayarisha malipo ya Msaada kwa ajili
ya Watoto Mayatima wanaosaidiwa na Shirika la Misaada la I,H,H,INSANI
YARDIM VAFKI kutoka Uturuki, hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya
Haile selasi mjini Unguja.
Baadhi
ya Watoto mayatima wanaopatiwa Fedha za Msaada na I,H,H,INSANI YARDIM
VAFKI kutoka Uturuki,wakishirikiana na Jumuiya ya Muzdalifat
wakiongozana na walezi wao kuchukua fedha zao.Zaidi ya watoto
800,wamepatiwa fedha hizo katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi mjini
Unguja.
Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Muzdalifat Farouk akizungumza machache katika
hafla ya kuwa kabidhi Fedha Watoto Mayatima Wanao fadhiliwa na Shirika
la I,H,H INSANI YARDIM VAKFI la uturuki,katika ukumbi wa Skuli ya Haile
Selasi Mjini Unguja.
Mfanyakazi
wa Jumuiya ya Muzdalifat akiwakabidhi Watoto mayatima Wanao fadhiliwa
na Shirika la I,H,H INSANI YARDIM VAKFI la uturuki,Fedha taslim za
msaada katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi Mjini Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
0 maoni:
Chapisha Maoni