Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza
katika halfa ya kuzindua mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP 2
2016-2021.
Katika
kuendeleza juhudi zake za kusaidia mataifa wanachama, Umoja wa Mataifa
(UN) umezindua mpango mpya wa misaada ya maendeleo nchini (UNDAP 2)
baada ya mpango wa kwanza wa UNDAP 1 kukamilika kwa mafanikio makubwa na
hivyo kuzinduliwa mpango mpya ambao utaendeleza hatua uliyoishia mpango
wa kwanza.
Katika
mpango huu mpya UN inataraji kutoa kiasi cha Dola Bilioni 1.3 ambazo
zitatumika katika kuboresha kusaidia kukuza uchumi na upatikanaji wa
ajira, kuboresha huduma zinazopatikana katika sekta ya afya, kuboresha
demokrasia, usawa wa kijinsia na haki za binadamu na kusaidia kupambana
na mabadiliko ya tabia ya nchini.
Akizungumza
katika halfa ya kuzindua mpango huo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez alisema utekelezaji wa mpango mpya wa
UNDAP 2 utakwenda pamoja na utekeleji na Malengo ya Maendeleo Endelevu
Duniani (SDGs).
Alisema
kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Tanzania katika
kusaidia upatikanaji wa huduma bora za kijamii na ni matumaini yake kuwa
wataendelea kudumisha ushirikiano uliopo sasa katika ya UN na serikali
ya Tanzania.
“Mpango
huu utaweka mbele vipaumbele vya taifa na utahakikisha kuwa hakuna mtu
ambaye anaachwa nyuma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa
Maendeleo Endelevu ambao unataka kila mtu ahusike,
“Umoja
wa Mataifa utaendelea kudumisha ushirikiano uliopo baina yake na
Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania pamoja na wananchi wake,”
alisema Rodriguez.
Nae
mgeni rasmi katika halfa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na
Katiba, Prof. Sifuni Mchome, alisema kuwa mpango huo umekuwa na matokeo
mazuri kwa Watanzania lakini pamoja na hilo pia serikali imekuwa
ikifanya jitihada mbalimbali zitakazoweza kukuza uchumi wa nchi na
wananchi wake.
Prof.
Mchome alisema kuwa serikali ya Tanzania inaushukuru Umoja wa Mataiffa
kwa kuwaletea mpango wa pili baada ya awali kumalizika lakini pia
serikali itahakikisha kuwa mpango huo utahusika kwa kila Mtanzania ili
na yeye aweze kufaidika na mpango wa UNDAP 2.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Prof. Sifuni Mchome akizungumza kwa niaba ya serikali katika uzinduzi wa UNDAP 2.
“Tunashukuru
baada ya ule wa kwanza mmetuletea mpango wa pili lakini pia hata pesa
imeongezeka kwa sasa kupata Dola Bilioni 1.3 kutoka ule wa kwanza ambao
ulikuwa wa Dola Bilioni 0.8 na katika mpango huu tutamshirikisha kila
mwananchi na yeye afaidike nao,
“Serikali
imekuwa ikifanya jitihada za kuleta maendeleo ya taifa na kwa mwananchi
mmoja mmoja lakini bado tunawahitaji wadau kama nyie na tunawaomba
msiondoke na tuendelee kufAnya kazi kwa kushirikiana,” alisema Prof.
Mchome.
Mpango
mpya wa misaada ya kimaendeleo ambao umetolewa na Umoja wa Mataifa (UN)
unataraji kuanza Julai, 2016 na kumalizika Juni, 2021.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima
akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dk. Juma Malik Akil akielezea jinsi UNDAP 1 ilivyosaidia sekta ya afya Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni