VIRUSI VYA UKIMWI vina ngazi zake katika mwili wabinadamu. moja yan tabia au ngazi ni kujigeuza geuza.
Virusi hivyo katika tabia yake ya
Nne, vinajigeuzageuza na kutokuwa kiumbe hai kwa wakati (They can stay in
dormany stage) yaani kama inavyokuwa mbegu za mazao.
Virusi hivi
vinashambulia kinga za mwili ambapo utendaji wa kinga za mwili ni sawa na
ulinzi wa nchi ingawa tofauti yake kubwa ni kwamba nchi tayari askari wapo lakini
mwili unaanza kutengeneza askari pale adui anapoingia na kisha hutuma
mashushushu.
Askari wa
mwili wanaitwa Antibodies na adui anaitwa antigen ambapo VVU humla askari
anayetumwa kufanya ushushushu waitwao CD4, hivyo taarifa sahihi hazipatikani
katika chuo cha kutengeneza askari na akitokea shushushu mmoja ametoroka bila
kuliwa, hupeleka taarifa ambazo haziwezi kufikia malengo ya kukabiliana na
adui.
Kipindi hiki
kidaktari huita kipindi cha mpito yaani kipindi cha dirisha la mpito (Window
period). Kipindi hiki mtu anaonekana mzima na hata akipimwa VVU havionekani.
0 maoni:
Chapisha Maoni