Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Said Amanzi,
amewataka wananchi kuacha chuki na migogoro isiyokuwa na tija dhidi ya
wawekezaji mbali mbali,kwa madai mambo hayo yanarudisha nyuma maendeleo
ya wilaya na mkoa kwa ujumla.
Amanzi
ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo
la kitega uchumi la Blue Plaza lenye ghorofa nne lillilo gharimu zaidi
ya shilingi 1.3 bilioni lililopo mtaa wa highway kata ya Majengo mjini
hapa.
Alisema kwa ujumla uwekezaji una faida nyingi ikiwemo ya kutoa ajira kwa vijana na watu wanaozunguka uwekezaji huo.
Alisema
pamoja na faida lukuki za uwekezaji,bado wapo baadhi ya wakazi wenye
chembechembe ya umwinyi ambao wakiona mwekezaji anapewa eneo la ardhi,
hujitokeza na kuanza kudai eneo hilo ni la babu yake hata kama eneo
husika lipo porini.
“Kumbukumbu
zinaonyesha kuna wakati hospitali kubwa ya St. Gasper inayomilikiwa na
kanisa la Roma Katoliki ilitarajiwa ijengwe katika kijiji cha Kisaki
manispaa ya Singida. Lakini baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kisaki
wakazua mgogoro ambao ulisababisha hospitali hiyo kujengwa Itigi. Sasa
hivi wakazi hao hao, wanafuata huduma za afya St. Gasper Itigi ambayo
ipo umbali mrefu”,alifafanua.
Akifafanua
zaidi, Amazni alisema wawekezaji wanapaswa kuungwa mkono na kusaidiwa
na wananchi wanaozunguka eneo la uwekezaji, ili wilaya na mkoa uweze
kupiga hatua zaidi katika kujiletea maendeleo endelevu.
Katika
hatua nyingine, DC huyo alisema mmiliki wa jengo la Blue Plaza bwana
Ponsian Rweyemela, ameonyesha njia kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa jengo
hili la kitenga uchumi ambalo litatoa ajira, litapendezesha mji wa
Singida na litaongeza mzunguko wa fedha.
“Kwa
ujumla Blue Plaza ni mali ya wakazi wa manispaa ya Singida na
Watanzania wengine watapata fursa ya kufanya shughuli zao zikiwemo za
biashara na kujiingizia kipato, wapo watakaoanzisha ofisi zao humu na
pia manispaa itapata ushuru/ kodi wa kutosha utakaolipwa na jengo hili.
Na Nathaniel Limu






0 maoni:
Chapisha Maoni