Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo
pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba,
mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba na kuahidi
kuyashughulikia. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omary
Makame.
Kamishna
wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame, akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya
kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao
yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkutano huo umefanyika Makao Makuu ya Polisi
Zanzibar.
Makamanda
wa Jeshi la Polisi na waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni katika
mkutano kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba,
mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba. (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
0 maoni:
Chapisha Maoni