Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua
akisoma maelekezo kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili ya Utumishi wa
Umma kwa wafanyakazi wa Ofisi yake jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni,
2016 (hawapo pichani) wakati wa maadhimishi ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanayoadhimishi kila mwaka Barani Afrika Juni 16-23.
Baadhi
ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa
maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoadhimishwa ofisi hapo.
Baadhi
ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa
Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na
Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoadhimishwa ofisi hapo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
……………………………………………………………………………………………..
Na. wandishi Wetu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua amewataka Wafanyakazi Ofisi ya
Waziri Mkuu kuzingatia maadili na kanuni za Utumishi wa Umma wakati wa
Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Dkt. Mwinyimvua amesema hayo
tarehe 22 Juni, 2016 Ofisini kwake Jiji Dar es salaam, wakati ofisi
yake ikiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kila mwaka
huadhimishwa Juni 16 – 23, 2016 Barani Afrika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi: Kuelekea katika Afrika tunayoitaka”.
“Kila mtumishi wa umma anapaswa
kuzingatia maadili na sheria za utumishi wa umma ambazo ndio nguzo ya
kuimarisha utendaji kazi na kuimarisha misingi na maadili ya Umma”
alisema Dkt. Mwinyimvua”.
Kuna sheria ya Utumishi wa Umma
ya mwaka 2002, maboresho ya Kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2009 na
miongozo mbalimbali inayoelekeza namna na jinsi mtumishi wa umma
anapaswa kuifuata.
“Nafahamu zipo changamoto nyingi
ambazo zinawapata watumishi wa umma nataka niwahakikishie kwamba,
serikali inazitambua na inazifanyia kazi hivyo nawasii tufanye kazi kwa
bidii kwani tunatambua kauli mbiu ya Serikali ya Mhe. Rais John Pombe
Magufuli ya Hapa Kazi tu inabidi kuitekeleza kwa kufanya kazi na tuache kufanya kazi kwa mazoea”, alisisitiza Dkt. Mwinyimvua.
Tumie mda wenu kujisomea vitabu,
Magazeti, Vijarida, vitawasaidia kujifunza na kupata maarifa tofauti
ambayo yataweza kuwasaidia kuwa wabunifu katika sehemu zenu za kazi,
elimu na maarifa inapatikana kwa kujisomea tujijengee mazingira hayo
yatawasaidia kuwaongezea ufanisi wa kazi, alisema Dkt. Mwinyimvua.
Kwa mwaka huu maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma yanaadhimishwa na Wizara na Taasisi za Serikali kwa
kukutana na watumishi wa umma na wadau mbalimbali kwa lengo la kupokea
changamoto, maoni, ushauri ikiwa ni lengo la Serikali la kutaka
kuboresha huduma kwa wananchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni