Jumatatu, 13 Juni 2016

Mikoa mitano yapata ugonjwa wa Kipindipindu, Morogoro waongoza wagongwa 43


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inaendelea na utaratibu wa kutoa taarifa ya mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa Kipindupindu nchini kila wiki kama tulivyoahidi, ili kutoa tahadhari kwa wananchi na maelekezo ya hatua za kuchukua ili kukabiliana na mlipuko huu.
Hadi kufikia tarehe 12 Juni 2016, jumla ya wagonjwa 21,786 nchini wametolewa taarifa,na kati yao Ndugu zetu 342 wamepoteza maisha tangu ugonjwa huu uliporipotiwa Agosti 2015.
Takwimu zinaonyesha kuwa, katika wiki hii inayoishia   tarehe 12 Juni 2016, Idadi ya wagonjwa walioripotiwa nchi nzima ni 78 na kati yao mmoja  alipoteza maisha.   Wiki iliyotangulia kulikuwa na wagomjwa 62 waliotolewa taarifa na kati yao watatu walipoteza maisha. Hii ikionyesha kuna ongezeko la wagonjwa walioripotiwa wiki hii ikilinganishwa na wiki iliyotangulia ingawa kuna kupungua 
Takwimu zinaonyesha kuwa, katika wiki hii inayoishia   tarehe 12 Juni 2016, Idadi ya wagonjwa walioripotiwa nchi nzima ni 78 na kati yao mmoja  alipoteza maisha.   Wiki iliyotangulia kulikuwa na wagomjwa 62 waliotolewa taarifa na kati yao watatu walipoteza maisha. Hii ikionyesha kuna ongezeko la wagonjwa walioripotiwa wiki hii ikilinganishwa na wiki iliyotangulia ingawa kuna kupungua 
kwa Idadi ya waliopoteza maisha.
Mikoa iliyoripoti ugonjwa wa kipindupindu wiki hii ni mitano(5), Morogoro ( wagonjwa 43 na kifo 1), Mwanza (21), Mara (7), Lindi (4) na Manyara (3).  Aidha wiki hii wilaya zilizoripoti ugonjwa wa Kipindupindu ni Morogoro vijijini (wagonjwa 27 na kifo 1), Morogoro mjini (8), Mvomero (8), Ilemela (12), Nyamagana (9), Tarime vijijini (5), Tarime mjini (2), Kilwa (4) na Simanjiro (3).  Mpaka sasa bado mikoa ya Njombe na Ruvuma    haijaripoti mgonjwa yeyote wa Kipndupindu tangu mlipuko huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka 2015
Licha ya kuwa kwa ujumla kasi ya  mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu imekuwa ikipungua,  takwimu hizi zinaashiria kuwa ugonjwa wa kipindupindu bado upo katika jamii tunazoishi na unagharimu maisha ya watu ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Hivyo wote kwa pamoja hatuna budi kuendeleza juhudi za ufuatiliaji na mapambano dhidi ya ugonjwa huu na tuendelee kutekeleza na kusimamia kikamilifu maelekezo na miongozo stahili inayotolewa na Wizara yangu.
Wizara yangu inaendelea kutoa onyo kali kwa Wasimamizi wa huduma za Afya Mikoani na katika Halmashauri, ambao wanaficha taarifa za wagonjwa wa Kipindupindu. Yeyote atakayebainika kuwa anaficha taarifa hizi atachukuliwa hatua kali. Wizara yangu inasisitiza kuwa, juhudi za kusimamia kikamilifu hatua mbalimbali za udhibiti wa mlipuko huu ziendelee.
Aidha katika kipindi hiki ambapo ugonjwa unaendelea kupungua,Wasimamizi wa huduma za Afya Mikoani na katika Halmashauri, waendelee kufuatilia na kuchunguza kwa kina, taarifa zote za vifo vinavyotokana na mgonjwa mwenye dalili za Kipindupindu kama kuharisha na kutapika. Taarifa hizi zinahitajika ili hatua madhubuti za kuzuia vifo ziweze kuchukuliwa.
Wizara inaendelea kuwapongeza na kuwashukuru wadau wote kwa jitihada za dhati zinazoendelea kutekelezwa na katika kusimamia kikamilifu miongozo inayotolewa na Wizara ili kuutokomeza ugonjwa huu, ikiwa ni pamoja na wataalamu wa sekta mbalimbali, Mashirika ya Kimataifa, Watumishi, Mikoa na Halmashauri pamoja na waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla.

0 maoni:

Chapisha Maoni