Kwanza Napenda kuchukua Nafasi hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuniwezesha kuiona siku ya Leo maana Si kwa uwezo wangu bali ni kwa Uwezo wake Muumba wetu aliye Juu.
Leo
ni siku muhimu sana kwangu maana inanikumbusha siku niliyoletwa Duniani
na Mungu kupitia Mama yangu kwa kusudi maalumu hapa duniani.
Napenda
Kumshukuru Mungu kwa maana neema na rehema zake ni Za milele. Nasema
asante kwa kunifanya kuongeza mwaka mwingine huku nikiwa na afya njema.
Kiukweli Sina cha Kumlipa Mwenyezi Mungu zaidi ya Kumsifu na Kumwabudu yeye kwa maana Sio kwa uwezo wangu.Napenda kuwashukuruni wote Ambao Mmekuwa mkiniombea na kunitakia heri ya kuzaliwa kwangu Nasema asante na Mungu awabariki sana.
Kiukweli Sina cha Kumlipa Mwenyezi Mungu zaidi ya Kumsifu na Kumwabudu yeye kwa maana Sio kwa uwezo wangu.Napenda kuwashukuruni wote Ambao Mmekuwa mkiniombea na kunitakia heri ya kuzaliwa kwangu Nasema asante na Mungu awabariki sana.
Nakukabidhi
wewe bwana njia zangu na kukutumainia kwasababu umeagiza kila
akukabidhie njia zake na kukutumainia unaenda kumtendea. Zaburi 37: 5
Leo nasema asante sana kwa Maana kila napokuita Wewe unaitika.
Naomba
pia uendelee kuziimarisha hatua zangu kwa maana uliagiza katika Zaburi
37:23 Kuwa “Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake”
Hakika wewe ni Mungu wa Wote.
Nachukua
fursa hii kuwa shukuruni wote Ambao mmenitakia baraka na heri katika
siku hii muhimu sana kwangu ambayo inanifanya nitafakari matendo yangu
hapa duniani, Uhusiano wangu na Mungu wangu, Uhusiano wangu na Ndugu
zangu, Uhusiano na Jamii yangu pamoja na rafiki zangu hakika Namshukuru
Mungu sana kwa kuniwezesha kupatana na Ndugu zangu, jamii yangu na hata
marafiki zangu. Kiukweli Namshukuru Mungu kwasababu Ni kwa neema zake na
Rehema zake ndio zimenifikisha hapa wala sio kwa ujanja wangu wala mimi
sio mwema sana kuzidi wengine.
Wewe
Ni Mungu wa wote, Huchelewi wala Huwahi Hakika nitakusifu na kukuabudu
siku zote za maisha yangu kwa maana matendo yako makuu uliyonitendea
Nayaona na kuyafurahia.
Asante
sana Mungu wangu naomba uendelee Kutimiza haja za Moyo wangu.
Nitaendelea Kukushangilia na Kukusifu kwa maana kila napokuita unaitika.
Happy Birthday to You Josephat Lukaza – Lukaza Blog
0 maoni:
Chapisha Maoni