Jumatano, 1 Juni 2016

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATEMBELEA MRADI WA UZALISHAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA GEREZA LA MTEGO WA SIMBA NA GEREZA KUU LA WANAWAKE KINGOLWIRA


kat1Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akipokea salaam kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, ACP. Shaban Kitolo mara tu baada ya kuwasili katika Gereza Mtego wa Simba katika ziara yake ya kikazi Mei 31, 2016, Mkoani Morogoro(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP, John Casmir Minja.
kat2Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP, John Casmir Minja(kulia) akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira kuelekea katika Shamba la uzalishaji wa ng’ombe wa maziwa la Gereza Mtego wa Simba.
kat3Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia kundi la ng’ombe wa maziwa katika shamba la uzalishaji wa ng’ombe wa maziwa Gereza Mtego wa Simba, Mkoani Morogoro. Gereza hilo hivi sasa linafuga ng’ombe wa maziwa 496.
kat4Kundi la ng’ombe wa maziwa wanaofugwa katika shamba la uzalishaji Mifugo Gereza Mtego wa Simba, Kingolwira Mkoani Morogoro wakiwa malishoni kama wanavyoonekana katika picha.
kat5Wafungwa wa Kike katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira(walioketi) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(meza Kuu) alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo ili kujionea uendeshaji wa Magereza hapa nchini.
kat6Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akionja chakula cha Wafungwa katika Jiko la Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira, Mkoani Morogoro alipofanya ziara ya kikazi ili kujionea Uendeshaji wa Magereza hapa nchini(kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP. John Casmir Minja.
kat7Sajini Taji wa Jeshi la Magereza, Sarah Kabunda ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Ufugaji Kuku katika Gereza Kuu la Wanawake Kongolwira akitoa maelezo ya Kitaalam kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira namna Ufugaji kuku unavyofanyika(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

0 maoni:

Chapisha Maoni