Jumanne, 7 Juni 2016

Marekani kuipa TZ msaada wa dola 800m


Uhusiano kati ya Marekani na Tanzania unaonesha dalili za kuimarika licha ya nchi hiyo kukatiza msaada wa awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) kwa Tanzania.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mheshimiwa Mark Childress amesema hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Bwana Childress alisema kuwa hivi karibuni ''kupitia shirika la misaada la Marekani, USAID tunatarajia kutia saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao.
''Aidha tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani na MCC.'' Alisema balozi Childress
"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha yanafanikiwa"
Rais Magufuli kwa upande wake alisema kuwa serikali yake itaendeleza kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani.

0 maoni:

Chapisha Maoni