Alhamisi, 2 Juni 2016

Mama Janeth Magufuli alipowasili mikoa ya Lindi na Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.

LIN1Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akimkaribisha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani huko kwa ajili ya Ziara ya kikazi katika mikoa ya kusini.
LIN2Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi na Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
LIN4Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na kinamama waliojitokea kumpokea alipowasili Mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.
LIN5Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akimshukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kuamua kufanya ziara ya kikazi mkoani humo.
LIN6Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiongea kwa niaba ya kina mama waliojitokeza kumpokea Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ambapo alimuahidi kuendelea kumuunga mkono kwenye shughuli zake na kumtaka kwenda mkoni humo mara kwa mara kwa ajili ya ziara za kikazi.Katikati mwenye pochi ya bluu ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
LIN8Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Ungo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
LIN9Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Kitenge Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.
LIN10Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Kitenge Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.
LIN11Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiwakabidhi zawadi ya mbuzi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kushoto) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa (katikati).
LIN12Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwashukuru kinamama na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea alipofika mkoani Lindi.
LIN13Mtoto Lulu Charles akimpa shada la maua Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipowasili Mkoani Mtwara.
LIN14Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali waliofika kumpokea alipowasili Masasi Mkoani Mtwara.
LIN15Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akimueleza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wake.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

0 maoni:

Chapisha Maoni