|
KATIKA
kukabiliana na suala la rushwa na ufisadi, serikali imetenga jumla ya Sh
bilioni 2.5 ili kuwezesha uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi. Aidha,
serikali imetenga jumla ya Sh bilioni 72.3 katika bajeti ya mwaka
2016/17 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kuiwezesha taasisi hii kutekeleza
majukumu yake kikamilifu.
Hayo yamo
katika Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, iliyowasilishwa
bungeni mjini Dodoma jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip
Mpango. Katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliweka
wazi kwamba itaanzisha mahakama maalumu ya kukabiliana na mafisadi na
wahujumu wa uchumi, na hivi karibuni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
alitangaza kwamba mahakama hiyo itaanza Julai mosi, mwaka huu.
Dk Mpango
alisema vile vile katika bajeti ya mwaka 2016/17, serikali imetenga Sh
bilioni 44.7 kwa ajili ya kuiwezesha Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAO)
kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kukagua na kudhibiti matumizi ya
fedha za umma.
0 maoni:
Chapisha Maoni