Imeelezwa
kuwa moja ya sababu ambayo inachangia kuwepo kwa tatizo la ajira nchini
basi ni maboresho ambayo yamekuwa yakifanywa na serikali katika sekta
ya elimu.
Hayo
yalielezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa katika kilele cha utoaji wa zawadi kwa
washindi wa shindano la Ajira Yangu Business Plan Competition
iliyohusisha vijana 831 na baadae kuchaguliwa 50 ambao waliishia katika
kinyang’anyiro hicho.
Bi.
Issa alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili
kuboresha elimu ya Tanzania lakini jambo hilo limekuwa likichangia
tatizo la ajira kwani kumekuwepo na ongezeko kubwa la vijana ambao
wamesoma lakini hawana ajira.
“Ukosefu
wa ajira kwa vijana hapa nchini ni changamoto iliyo wazi ambayo
imechochewa kwa kasi kubwa na mabadiliko ya kisera na kiuchumi
yanayosimamiwa kwa dhati na Serikali katika kupeleka mbele zaidi Taifa
letu kiuchumi na kijamii,
Mgeni
Rasmi Beng’i Issa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC) akitoa hutuba wakati wa sherehe za kugawa zawadi kwa
washindi wa shindano la Ajira Yangu siku ya Jumatatu ya tarehe
13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi
Duniani (ILO).
“Maboresho
ya mfumo wa elimu nchini kama vile upanuzi wa elimu ya msingi na
sekondari umechochea kukua kwa kasi kwa kundi kubwa la vijana
wanaomaliza elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu,” alisema Bi.
Issa.
Aidha
aliwataka vijana ambao wamepata nafasi ya kuendelezwa mawazo yao
kupitia shindano hilo kutumia vyema fursa hiyo kwa kuendeleza mawazo ya
biashara ambayo walikuwa nayo ili yaweze kuwasaidia kubadilisha hali za
maisha yao.
Pia
alitumia fursa hiyo kuziomba taasisi za kifedha ambazo zinatoa mikopo
kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia vijana kutokana na taasisi
nyingi kuwa na uataratibu ambao ni mgumu kwa vijana na kuwaeleza kuwa
NEEC ipo tayari kushirikiana nao ili kutazama ni jinsi gani wanawezesha
jambo hilo kufanikiwa.
Dr.
Mary Kawar, Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Kazi Duniani (ILO) akiongea na
vijana pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi rasmi wa sherehe za
kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la kuandaa michanganao ya
kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu. Sherehe hizo zilifanyika
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kukutanisha Zaidi ya
vijana 400 kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kongamano hilo liliandaliwa
kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa
ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Eugene
Mkami, mmoja wa washiriki waliofikia hatua ya 20 bora akieleza mawazo
yake ya biashara mbele ya jopo la majaji na washiriki waliohudhuria
kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena siku ya
tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika
la Kazi Duniani (ILO).
Dr.
Sebastian Ndege, mjasiriamali na Mkurugenzi wa Ndege Insurance Brokers
(wa kwanza kushoto), Modesta Lilian Mbughuni, mjasiriamali na
mwanzilishi wa The Professional Approach Group (katikati) na Ruge
Mutahaba, Mkurugenzi wa Clouds Media Group wakijadili mada katika
kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena siku ya
tarehe 13/06/2016.
Paul
Mashauri, mjasiriamali na mwanzilishi wa Masterclass Worldwide (wa
kwanza kushoto) Mercy Kitomari, mjasiriamali na mwanzilishi wa NELWA
Gelato ( katikati) na Immaculate Steven, mjasiriamali na mwanzilishi wa
Lavender Catering ( wa kwanza kulia) wakisikiliza kwa makini maswali
kutoka kwa vijana wakati wa kongamano la Ajira Yangu lililofanyika
katika hoteli ya Serena siku ya tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo
liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirima la Kazi Duniani (ILO).
Eng.
Omari Bakari, Mkurugenzi Mkuu, SIDO akizungumza na vijana wajasiriamali
wakati wa kongamano la Ajira Yangu lililokutanisha vijana zaidi ya 400
kutoka mikoa mbalimbali nchini.Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano
na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Lilian
Madeje (wa kwanza kushoto, Daudi Mbaga, Mkurugenzi wa Masoko UTT (wa
pili kushoto), Elia Yobu kutoka Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (wa pili kulia na Abella Betayunga, mjasiriamali wakizungumzia
namna ya kupata fedha za kuendeshea biashara wakati wa kongamano la
Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena jumatatu tarehe
13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la
Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi
Duniani (ILO).
Baadhi
ya washiriki wakifuatilia kwa makini michango ya watoa mada wakati wa
kongamano kubwa la wajasiriamali vijana Kongamano hilo liliandaliwa kwa
pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa
ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Mmoja
wa washiriki wa kongamano la Ajira Yangu akiuliza swali kwa
muwasilishaji wakati wa zoezi la maswali na majibu katika kongamano
kubwa la wajasiriamali vijana lililofanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam jumatatu ya tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo
liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Albert
Sanga, mjasiriamali katika sekta ya kilimo na mwanzilishi wa Bunge la
Uchumi akizungumza na washiriki wa kongamano la Ajira Yangu
lililofanyika katika hoteli ya Serena siku ya jumatatu tarehe
13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi
Duniani (ILO).
Nancy
Lazaro (kushoto) kutoka Shirika la Kazi duniani (ILO) pamoja na Lilian
Madeje wendesha shughuli (kulia) wakitaja jina la mmoja wa washindi wa
mchezo wa bahati nasibu uliuochezeshwa ukumbuni hapo ili kupata mshindi
atakayepata fursa mbalimbali zinazotolewa Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bing’i
Issa, wa kwanza kushoto na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani
Mary Kawar, wa kwanza kulia, wakimkabidhi mfano wa cheki yenye thamani
ya fedha za kitanzania 15,323,000/=kijana Gilbert Tarimo wa Inoge Rabbit
Farm baada ya kuibuka mshindi namba moja kwa wajasiriamali wanaoanza
katika shindano la michanganuo ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira
Yangu lililoratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
(NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Shindano hilo
lilihusisha zaidi ya michanganuo ya kibiashara 800 kutoka kwa vijana
mbalimbani nchini.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Bing’i
Issa, wa kwanza kushoto na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani
Mary Kawar, wa kwanza kulia, wakimkabidhi mfano wa cheki yenye thamani
ya fedha za kitanzania……kijana Linda Nasson baada ya kuibuka mshindi
namba nne kwa wajasiriamali wanaokua katika shindano la michanganuo ya
kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu lililoratibiwa na Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushiriano na Shirika la
Kazi Duniani (ILO). Shindano hilo lilihusisha zaidi ya michanganuo ya
kibiashara 800 kutoka kwa vijana mbalimbani nchini.
Bing’i
Issa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)
na Mary Kawar, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO)
wakigawa cheti kwa mmoja wa washiriki waliovuka hatua ya 20 bora katika
shindano la kuandaa michanganao ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira
Yangu. Sherehe hizo zilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam na kukutanisha Zaidi ya vijana 400 kutoka mikoa mbalimbali
nchini. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la
Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi
Duniani (ILO).
Dr.
Mary Kawar, Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa pili
kulia na Bing’i Issa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC) wakigawa cheti kwa mmoja wa washiriki waliovuka hatua ya
20 bora katika shindano la kuandaa michanganao ya kibiashara
lijulikanalo kama Ajira Yangu. Sherehe hizo zilifanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam na kukutanisha Zaidi ya vijana 400 kutoka
mikoa mbalimbali nchini. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na
Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano
na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Baadhi
ya vijana wakiangalia bidhaa za mmoja wa washiriki wa shindano la Ajira
Yangu lililoshindanisha michanganuo ya biashara wakati wa kilele cha
shindano hili kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano
na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Baadhi
ya vijana wakiangalia bidhaa za mmoja wa washiriki wa shindano la Ajira
Yangu lililoshindanisha michanganuo ya biashara wakati wa kilele cha
shindano hili kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano
na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
0 maoni:
Chapisha Maoni