Kila
Juni 16 ya mwaka Bara la Afrika linaadhimisha sikiu ya mtoto wa Afrika,
tunapoadhimisha kumbukumbu ya siku ya mtoto wa Afrika ambapo pia kwa
mwaka huu 2016 ikiwa ni mara ya 26 tangu uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za
Afrika (OAU) uizindue siku hiyo mwaka 1991,
kwa kuona umuhimu wa siku hii, Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya
Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) imeweza kushirikii
tukio hilo pamoja na kucchangia kiasi cha fedha.
Katika
ushiriki huo, Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya Umma na masoko UTT-PID,
Bi. Eugenia Simon alieleza kuwa UTT-PID kwa kuona umuhimu wa siku ya
Mtoto wa Afrika wameonelea kuchangia siku hiyo kwani ni faraja kwa
watoto wote.
Aidha,
Bi. Eugenia aliweza kutoa mfano wa Hundi kwa watendaji wa mji mdogo wa
Chalinze kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya watoto wa mji huo.
UTT-PID
pia inaendesha miradi yake ya viwanja katika Mkoa huo wa Pwani ikiwemo
mji wa Chalinze na Bagamoyo. Ambapo katika mji huo wa Chalinze, UTT-PID
ina mradi wa upimaji na uuzaji wa viwanja ujulikanao kama New Chalinze City huku ule wa Bagamoyo ukijulikana kama New Mapinga City.
Mkuu
wa kitengo cha Mahusiano ya Umma na masoko UTT-PID, Bi. Eugenia Simon
(wa kwanza kulia) akifuatilia maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa
Afrika katika mji wa Chalinze jana Juni 16.2016
Mkuu
wa kitengo cha Mahusiano ya Umma na masoko UTT-PID, Bi. Eugenia Simon
akitembezwa katika moja ya mabanda yaliyokuwa yakionyesha bidhaa katika
siku hiyo.
Maadhimisho hayo yakiendelea.
Mkuu
wa kitengo cha Mahusiano ya Umma na masoko UTT-PID, Bi. Eugenia Simon
akielezea maneno machache namna ya taasisi hiyo inavyofanya shughuli
zake hapa nchini
Mkuu
wa kitengo cha Mahusiano ya Umma na masoko UTT-PID, Bi. Eugenia Simon
akikabidhi hundi ya fedha kwa Mtendaji wa Chalinze kwa ajili ya watoto
wa mji huo. (Picha zote na UTT-PID).
0 maoni:
Chapisha Maoni