JESHI la Polisi Mkoa wa
Kaskazini Pemba limewatoa hofu wananchi katika Mkoa huo wanaotekeleza
ibada ya usiku wakati huu wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan kwamba ulinzi
umeirishwa .
Kamanda wa Polisi Mkoa huo
kamishna msaidizi mwandamizi , Hassan Nassir Ali amesema , tayari kikosi
cha usalama barabarani kimeongezwa nguvu kwa kuongezewa watendaji ili
waweze kuyafikia maeneo yote.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi Ofisini kwake ja ameahidi kuimarisha ulinzi wa wananchi
pamoja na mali zao kwa kipindi chote cha mfungo wa mwezi wa Ramadhan kwa
kuongeza maradufu doria za kawaida .
Aidha ameeleza kuwa ulinzi
umeiramishwa zaidi katika maeneo ya miji ya Wete , Konde na Micheweni na
kuwatoa hofu wananchi wanaotekeleza ibada ya usiku wakati huu wa mfungo
wa mwezi wa Ramadhan .
Pia Kamanda Hassan Nassir Ali
amezidi kuwahakikishia wananchi kuwa jeshi la Polisi litaendelea
kutunza siri wanazozitoa na kuwataka kutoa ushirikiano ili kufanikisha
malengo yaliyokusudiwa .
“Napenda kuwahakikishia
wananchi kuwa jeshi la Polisi litaendelea kutunza siri na taarifa ambazo
wanazitoa , hivyo ni vyema kuendelea kutupa taarifa ambazo
zitafanikisha kuwadhibiti wanaopanga njama ya kufanya hujuma
”alifahamisha.
Amesema utaratibu huo
ulioandaliwa na Jeshi la Polisi umelenga kupunguza matukio ya kihalifu
pamoja na yale ya ukiukwaji wa kanuni na sheria za nchi hususani za
usalama barabarani .
Akizungumzia tabia ya baadhi ya
askari kuvujisha siri wanazopelekewa na raia wema , amesema kwamba ni
vyema wananchi kuwasiliana moja kwa moja na wakuu wa Vituo pamoja na
maofisa wengine wa jeshi kuwaripoti askari wanaotoa siri ili wachukuliwe
hatua za kisheria .
“Ni vyema wananchi kuwasiliana
moja kwa moja na maofisa wa Jeshi la Polisi kuwaripoti Askari ambao
wanavujisha siri , kwani wanalipaka matope jeshi na kwamba
tutawachukulia hatua za kisheria ”alisisitiza.
Amesema askari hao
wanasababisha Jeshi kulaumiwa na wananchi , na kuwafanya wananchi wakose
imani na chombo chao cha ulinzi kutokana na askari wachache wanaokiuka
maadili ya kazi zao .
0 maoni:
Chapisha Maoni