wenyekiti wa Chama cha UDP Mzee
John Momose Cheyo akimpongeza mke wa Goodluck Joseph Ole Medeye mara
baada ya mume wake kujiunga na Chama cha UDP leo.
……………………………………………………………………………………………………………………..
Kada wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA, aliyedumu na chama hicho kwa miezi kumi na moja
Goodluck Ole Medeye, amekihama chama hicho na kujiunga na United
Democratic Party UDP.
Bw. Medeye aliyewahi kuwa
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na kuitumikia serikali katika
nafasi ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
ametangaza uamuzi wa kuhama Chadema jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa
kadi ya UDP na Mwenyekiti wa Chama hicho John Momose Cheyo.
Mbunge huyo wa zamani wa jimbo la
Arumeru Magharibi amejiunga na UDP akiwa na Mkewe, pamoja na watu
wengine tisa wakiwemo waliokuwa kwenye vyama tofauti na wengine waliodai
hawakuwahi kuwa kwenye siasa, ambapo katika maelezo yake, Ole Medeye
amesema awali alitaka kuunda chama kipya lakini baada ya kupitia katiba
za vyama akaona UDP ni sehemu sahihi.






0 maoni:
Chapisha Maoni